Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akiwasili katika Kata ya Msalato kwa ajili ya kuzungumza na wanawake wa Kata ya hiyo alipofanya ziara ya kata kwa kata kwenye vikao vya ndani.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akisisitiza jambo kwa wanawake wa Kata ya Msalato alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Msalato alipofanya ziara ya kata kwa kata kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kufanya vikao vya ndani.
Wanawake wa Kata ya Msalato wakimsikiliza Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa (hayupo pichani) alipofanya kikao nao kuwaeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwenye awamu ya kwanza ya Rais Magufuli pamoja na kumuombea Kura
Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini,Diana Madukwa akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Msalato,Bw.Nsubi Bukuku kwa wanawake wa Kata ya Msalato.
……………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa ameendelea na ziara ya kufanya vikao vya ndani kwa kuwaombea kura za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM kwa wanawake wa kata ya Msalato.
Madukwa, amewaomba wanawake hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 wakiwa na vitambulisho vyao vya mpiga kura ili waweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.
Madukwa amesema kwa miaka mitano ya Dk Magufuli wanawake wamenufaika na mikopo ya serikali inayotolewa kwenye Halmashauri zote nchini ambayo imekua haina riba wala makato yoyote jambo ambalo limewafanya kina mama wengi kupiga hatua za kimaendeleo.
” Dodoma sisi tumefaidika sana na Dk Magufuli kwanza ametuheshimisha kwa kuleta Makao Makuu ya Nchi hapa, wizara zote na taasisi ziko Dodoma hii ni fursa kubwa sana kwetu, ametujengea soko na stendi kubwa ambayo itakua chanzo cha mapato kwa Jiji letu, niwaombe Oktoba 28 mjitokeze kwa wingi mkapige kura.
Dodoma ya leo siyo kama ya zamani, miaka mitano nyuma tulikua hatuna barabara za lami tulizonazo leo, Dk Magufuli amepambana na changamoto zetu kwa kiasi kikubwa na amefanikiwa, tusimvunje moyo, tukampe kura nyingi za kishindo,” Amesema Madukwa.
Aidha Madukwa amewataka wanawake hao kutokubali kutoa vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa watu wanaopita kwenye maeneo yao wakiahidi kuwapatia mikopo.
Madukwa amaesema kuwa kuna watu wameanza kupita wanachukua vitambulisho hivyo wakiahidi kuwapatia mikopo jambo ambalo si kweli kwa kuwa wamekuwa wakichukua na kwenda kutengeneza nakala inayofanana na kitambulisho hicho.
“Hawa wanachukua na kwenda kutoa ‘copy’ ambayo inakuwa ngumu kama kitambulisho, siku ya kwenda kupiga kura unakuta tayari ulishapiga kura kumbe hujapiga, ndugu zangu msikubali kuwapa watu hao wanaokusanya vitambulisho kitambulisho ni haki yako wewe kwa hiyo nawakumbusha mkatunze vitambulisho vyenu,”amesema Madukwa