Wataalam wa Wizara ya Maji wakikagua bomba katika mradi wa maji wa Kirando, bomba hilo litakalotoa maji katika ziwa Tanganyika na kuyasafirisha hadi katika tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja, na kuweza kuhudumia wananchi zaidi ya elfu 40 katika vijiji saba vya Nkasi kwa asilimia 100.
Jengo ambapo itafungwa pampu katika chanzo cha mradi wa maji wa Kirando kilichopo Ziwa Tanganyika. Mradi huu utafikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wananchi wa Nkasi kwa asilimia 100 na umetekelezwa kwa utaratibu wa force account, kwa kutumia wataalam wa sekta ya maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA) Mhandisi Gibon Nzowa (kati kati) akikagua kazi ya uunganishwaji wa bomba la kutoa maji katika chanzo cha mradi kupeleka katika tanki. Mradi huo unasimamiwa na SUWASA na umefika asilimia 85 ya utekelezaji.
Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (katikati), akijadiliana na wataalam kuhusu utekelezaji wa mradi wa Kirando ambao upo katika hatua za mwisho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA) Mhandisi Gibon Nzowa na kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Maji Bi. Mwajuma Lugendo
Sehemu ya juu kabisa ya tanki la mradi wa maji wa Kirando litakalohudumia wakazi wa wilayani Nkasi, likiwa limekamilika, ujenzi wake umefanyika katika vilima vya ziwa Tanganyika.
……………………………………………………………………………….
Wakazi wa Nkasi wana kilasababu ya kufurahi baada ya mradi wa maji wa Kirando utakaohudumia zaidi ya wananchi elfu 40 kufika katika hatua za mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA) Mhandisi Gibon Nzowa amesema kazi zilibaki zitakamilika ndani ya muda mfupi, na majaribio ya mradi huo yataanza.
Mradi wa maji wa Kirando unaotekelezwa na wataalam wa sekta ya maji kwa utaratibu wa force account, unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).
Pamoja na kazi nyingine, mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja, na chanzo cha maji ya mradi ni Ziwa Taganyika, ambapo vijiji saba vya Nkasi vitapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa asilimia 100.