Na John Walter-Manyara
MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Umbura amewaomba wakina mama mkoani humo kupiga kura za kishindo kwa Rais Magufuli na Wagombea wote wa Chama hicho.
Umbura amesema kuwa kwa mengi yaliyofanywa Mkoa wa Manyara na Rais John Magufuli, zawadi pekee ya kumpa ni kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Amewataka wananchi wote Mkoa wa Manyara kuhakikisha wanapiga kura zote kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi.
Umbura amesema haoni sababu ya Dk. Magufuli kutompa miaka mingine mitano, kwani ameonesha dhahiri kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita nia yake ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora kwenye afaya, Elimu na kuboresha Miundombinu.