Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM akiwasalimia viongozi mbalimbali pamoja na Wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar wakati akitokea Tunduma mkoani Songwe.
**********************************
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameongoza mapokezi ya kumpokea mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mapokezi hayo, yamefanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar leo tarehe 02 Oktoba, 2020 ambapo Mhe. Dkt. Magufuli ameeleza kwa ufupi,
“Leo nimeingia hapa Zanzibar, nimeingia Zanzibar kwa ajili ya kuja kufanya Kampeni, kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi.”
Mgombea wa Urais wa CCM Mhe. Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni kesho tarehe 03 Oktoba, 2020 katika viwanja vya Mnazi mmoja Mkoa wa Mjini.