Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya maili moja ikiwa ni moja ya kampeni zake kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi waweze kumchagua tena katika kuongoza katika kipindi cha miaka mitano mingine.
Mgombe Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka wa kushoto kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) wakiwa sambamba kwenye jukwaa na mgombea udiwani wa Kata ya maili moja Ramadhani Lutambi katika mkutano wa kampeni kwa ajili ya kutoa sera zao kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mmoja kati ya makada wa chama cha mapinduzi Mjema wa kushoto akiwa amesimama jukwaani huku amemshika mkono kwa ajili ya kumandi mgombea udiwani wa kata ya maili moja Ramadhani Lutambi wa kulia katika mkutano wa kampeni amabo ulifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Bundikani.
Baadhi ya wagombea wa nafasi mbali mbali wakiwa wanatoa sera zao kwa wananchi wa kata ya maaili moja kwa ajili ya kuwapa fursa nyingine ya kuwachaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kushoto ni Mgombea ubunge wa jimbo la kibaha Syvestry Koka na kulia kwake ni mgombea udiwani kata ya maili moja Ramadhani Lutambi.
Mwonekano wa picha ya Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Syvestry Koka wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi kwa ajili ya kuweza kujinadi pamoja na kuomba kura kwa wananchi waweze kuwachagua.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Maulid Bundala akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya maili moja hawapo pichani kwa ajili ya kuzungumzia sera na ilani ya chama sambamba na kuwanadi wagombea wa nafai ya Urais, Ubunge pamoja na Udiwani.
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM ambao walifika katika mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya kusikiliz sera za wagombea mbali mbali katika nafasi za ubunge pamoja na udiwani,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………………
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mji kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Sylvestry Koka amesema endapo atachaguliwa na wananchi kuwaongoza tena katika kipindi kingine cha miaka mitano atahakikisha analivalia njuga suala la kukabiliana na changamoto inayowakabiliwa wakinamama wajawazito kupoteza maisha wakati wa kujifungua kwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kununua vifaa tiba vya kisasa.
Koka aliyasema hayo wakati wa kampeni ya kuomba kura kwa wananchi wa maeneo ya mbali mbali ya bundikani katika kata ya Maili moja ambapo amebainisha kwamba nia yake kubwa ni kuendelea kushirikiana na wananchi na serikali ambayo itaingia madarakani katika kuweka mazingira rafiki katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi husussan wakinamama wajawazito.
“Ndugu zangu wananchi pamoja na kuwepo kwa mambo mbali mbali ya kimaendeleo ambayo nimeshakwishayafanya lakini tumekuwa na mradi mwingine wa Kijimbo ambapo tumeweza kushirikiana na serikali kwa kujenga jengo kubwa la kisasa kwa ajili ya kujifungulia wakinamama ambalo limejengwa pale katika hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi haya ni moja ya juhudi zangu katika kuboresha afya,”alisema Koka.
Aidha mgombea huyo alibainisha kwamba kutokana na kuwepo na changamoto ya upatikanaji wa wa utoaji wa huduma katika baadhi ya maeneo alipambana vilivyo mnamo mwaka 2012 kwa ajili ya kuomba ujenzi wa mradi wa hospitali mpya ya Wilaya ambapo maombi yake yaliweza kuzaa matunda kutokana na mradi huo kukamilia.
“Wakati nipo katika nafasi yangu ya Ubunge mnamo mwaka 2012 niliomba ujenzi wa hospitali ya Wilaya lakini alivyoingia katika kipindi kingine aliweza kupambana kutokana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa hospitali hiyo ambayo itaweza kuwa mkombzo mkubwa kwa wananchi kupatiwa matibabu yao kwa urahisi na kwamba kwa sasa hospitali hiyo imekamilika na tayari imeshaanza kutoa huduma,”alisema Mgombea huyo.
Kadhalika Koka alisema kwamba katika kuboresha sekta ya afya wakati akiwa Mbunge alishatoa msaada wa vifaa tiba mbali mabli katika kituo cha afya ya Mkoani lengo ikiwa ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuhakikisha anasimamia vema suala zina la upatikanaji wa dawa ili wananchi waweze kupata matibabu bila usumbufu wowote.
Akizungumzia kuhusiana na suala la mipango yake katika kuboressha sekta ya afya aliongeza kuwa anatambua bado kuna baadhi ya maeneo mengine kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma ya aafya hivyo amewaomba wananachi waweze kumpatia ridhaa ya kuongoza katika kipindi kingine ili aweze kumalizia utekelezaji wa ilani ya chama katika kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi.
Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya Maili moja kupitia tiketi ya ( CCM) Ramadhani Lutambi alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anasimama kidete katika kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya barabara pamoja na kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga na kukarabati madarasa katika shule za msingi na sekondari.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi katika Halmashauri ya mji Kibaha Maulid Bundala alibainisha kwamba amewaomba wananchi kuhakikisha wanafanya maamuzi yaliyo sahii kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM wenye uwezo wa kusikiliza kero za wananchi na kuleta maendeleo.