**********************************
Na Woinde Shizza, Arusha
Mahakama kuu kanda ya Arusha,masijala ndogo ya kazi imetoa hati ya kukamata kwa jenereta kubwa mbili aina ya Katapila Mali ya hotel ya Ngurdoto ambaye ni mdaiwa kwenye shauri la madai namba 98/2018 ili kufidia deni linalotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi .
Akitoa amri hiyo mahakamani hapo msajiri wa mahakama hiyo, John Mkwabi alisema mahakama imepokea maombi ya upande wa mashtaka na kutoa hati ya kukamatwa kwa jenereta hizo ili kufidia malipo ya sh,milioni 231,000,000 yanayotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.
Awali afisa kazi mkoa wa Arusha,Emmanuel Mweta alisema kuwa awali Mali zilizokuwa zimeombwa kukamatwa ni magari mawili ambayo yamebainika kutokuwepo kwenye kumbukumbu ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA kama ni Mali za mdaiwa .
“Mheshimiwa msajiri tunaiomba mahakama tubadilisha Mali za kukamatwa kwa mdaiwa baada ya magari mawili tuliokuwa tumeomba kutokuwemo kwenye kumbukumbu ya TRA na hivyo tunapendekeza Mali nyingine ambayo ni jenereta mbili aina ya katapila lenye ukubwa wa umeme wa KV 400 ambayo ni Mali ya mdaiwa” Alisema Mweta.
Pia Mweta alitoa maombi ya kupata hati ya kuvunja sehemu ya jengo la hotel ya Ngurdoto iliyokuwa imejengewa jenereta hilo ili liweze kutolewa .
Hata hivyo msajili Mkwabi aligoma kutoa hati Mara mbili na kutoa Maelezo ya kuendelea na zoezi hilo na kama kutakuwa na tatizo mdaiwa atapaswa kufika mahakamani .
Shauri hilo limeahirisha hadi litakapo tajwa tena tarehe 27,Oktoba mwaka huu ,hata. Hivyo msajiri aliagiza utekelezaji wa ukamataji wa jenereta hizo uwe umekamilika ifikapo Oktoba 20 mwaka huu.
Wakati huo huo mahakama hiyo imeamuru kuuzwa kwa Mali za mdaiwa ambaye ni Hotel ya Naura Spring zinazoshikiliwa na dalali wa mahakama na zoezi hilo liwe limekamilika ifikapo Novemba 17,mwaka huu.
Aidha mahakama hiyo imetoa oda ya kukamatwa kwa jenereta na gari moja aina ya Noar lenye Namba T 991 BWD Mali ya mdaiwa ili kufidia deni la sh,milioni 32,000,000/linalotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.
Maombi ya kukamata Mali hizo yametolewa mahakamani hapo na afisa kazi,Emmanuel Mweta ambaye aliiambia mahakama katika shauri la madai namba 83/2019 kwamba Mali zilizokuwa zimeombwa hapo awali zinathamani kubwa na hivyo kuiomba mahakama hiyo kukamata Mali zingine.
Pia Mweta aliiomba mahakama hiyo kumpangia tarehe ya mnada wa kuuza magari matatu yanayoshikiliwa na dalali wa mahakama .
Wakili anayemwakilisha mdaiwa,Herode Biliamutwa alidai hana pingamizi na maombi hayo,ndipo msajiri wa mahakama hiyo John Mkwabi alipoamuru ifikapo novemba 12,mwaka huu Mali zilizokuwa zimepatikana ziwe zimeuzwa.
Shauri hilo limeahitishwa hadi novemba 2020 mwaka huu litakapotajwa tena.