Home Mchanganyiko MFANYAKAZI WA TANESCO AMKATA MKE WAKE KIGANJA CHA MKONO

MFANYAKAZI WA TANESCO AMKATA MKE WAKE KIGANJA CHA MKONO

0

*******************************

Na Woinde Shizza 

Mfanyakazi wa shirika la umeme Tanesco jijini Dar es salaam Ombeni Alfayo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kitendo kukata mkono mkewe na kusababisha kiganja Cha mkono wa kulia kutengana na sehemu nyingine ya mkono
Akiongeza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni   Alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya Saa 5:45 asubuhi maeneo ya siwandeti ,Iliopo kata ya Kiranyi Tarafa ya Enaboishu wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha Ambapo  alimkata mke wake Veronica Kidemi (30)mmasai na mwalimu wa shule ya sekondari Kiranyi na mkazi wa siwandeti ambapo alimjeruhi kwa kumkata na kitu chenye ncha Kali katika mikono yake miwili
Alisema kuwa uchunguzi unaendelea  Ili kubaini chanzo Cha tukio hilo ingawa taarifa za awali zinasema kuwa chanzo Ni wivu wa kimapenzi ,ambapo aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikimbia Mara Baada ya kufanya tukio hilo na tayari ameshakamatwa katika jiji la Dar es salaam Mara Baada ya upelelezi kukamilika na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria aidha pia majeruhi amelazwa katika hospital ya selian-ngaramtoni
Akiongelea tukio hilo mwalimu huyo Veronica Kidemi Alisema kuwa mume wake huyo alikuwa anamtishia Mara kwa Mara ,na alikuwa akimpiga Mara kwa Mara  na inatokana na wivu alionao mume wake 
“Aliniita kutokea kazini nikaenda nilipotoka nikamkuta amejificha jikoni ndio akaanza kunikimbiza na kunikatakata mapanga hapa unapoona mkono unaniuma huu mmoja na huu mungine nimewekewa chuma ” Veronica
Kwa upande wake daktari bigwa wa mifupa wa hospital  Seliani Robert Julius amethibitisha kumpokea akiwa anavuja damu nyingi na wakaanza kumpatia  matibabu na kwa Sasa anaendelea vizuri.