Meneja wa Mafunzo na Utafiti wa TBS Bw. Hamisi Sudi, akitoa elimu ya vifungashio bora kwa wadau wa mafuta ya kula katika Manispaa ya Tabora.Wazalishaji wa mafuta ya kula wakifuatilia mafunzo katika Manispaa ya Tabora
*************************************
NA MWANDISHI WETU
Takwimu zinaonesha mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni tani laki nne kwa mwaka wakati uzalishaji unaofanyika ni tani laki mbili kwasasa hivyo Serikali imamua kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa mafuta ya kula ili kuongeza wingi wa mafuta hayo kwa mahitaji ya nchi.
Ameyasema hayo leo Meneja wa Utafiti na Mafunzo kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS, Bw.Hamis Sudi wakati wa utoaji mafunzo kwa wazalishaji wa mafuta ya kula Mkoani Tabora.
Akizungumza Mkoani humo,Bw.Sudi amesema kuwa utoaji wa mafunzo kwa wazalishaji hao utaongeza nguvu kwa uzalishaji wa mafuta hayo kwasababu mngin yankuwa yanaota katika mnyororo mzima wa uzalishaji.
“Tunatumia fursa hii kuwalezea majukumu ya TBS ikiwa na pamoja na yale ambayo yalikuwa yanafanywa na TFDA majukumu hayo ni pamoja usajili wa vyakula na vipodozi lakini na majengo,wale watu wa mabucha,migahawa,surpmarketi na wale wenye maghala kwamba ni namna gani shuguli zile zinazofanywa na TBS, na kimsingi ufanisi wa kazi bado upo”.Amesema Bw.Sudi.
Amesema kwenye mafunzo hayo wanawashirikisha wataalamu kutoka SIDO pamoja na mwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ia wanatumia wenyeji wao kufanikisha zoezi hilo.
Pamoja na hayo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za kibiashara ili waweze kupata majawabu na kuweza kuzalisha bidhaa iliyobora na kuweza kupata masoko makubwa na uzalishaji kuongezeka.
Mpaka sasa washafikiwa wadau zaidi ya 680 katika mikoa ya Singida na Tabora.