Sehemu ya Matofali yaliotolewa na Tretem Network of School
Ujenzi wa moja ya Darasa ukiendelea
……………………………………………………………………….
NA FARIDA SAIDI,MOROGORO.
Katika kuunga mkono juhudi zinzofanywa na serikali,Jamii imetakiwa kuchangia miradi ya maendeleo inayofanywa katika maeneo hususani miradi ya elimu ili kuwapa fursa watoto kusoma katika mazingira mazuri na salama yatakayochochea ufauru.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaaji wa Tretem Network Of School Geofrey Chami wakati anakabidhi matofali miatano(500) kwa Mkuu wa shule ya msingi shikizi ya Tungi iliopo kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro,ambapo tofali hizo zitasaidia kumaliza kujenzi wa dalasa moja ambalo lipo katika kahatua ya awali.
Aidha amewataka wadau wengeni kujitokeza katika kusaidia ujenzi wa madarasa yaliobaki pamoja na mahitaji mengine yanayohitajika katika shule hiyo ikiwemo madawati,huku akisema jukumu la kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira salama ni wote nasio serikali pekee.
Kwa upande wao Mkuu wa shule hiyo na Mwenyekiti wa mtaa wameishuru Taasisis ya Tretem Network Of School kwa kutoa matofali hayo ambayo wanaamini yatakuwa chachu ya kuwasukuma wadau wengine kusaidia shule hiyo shikizi.
Hata hivyo shule hiyo ni shikizi kutoka shule ya msingi tungi ambayo ndio shule mama na imeanzishwa hivi karibuni kwa lengo la kuwasidia watoto wanasoma umbali mrefu katika kata hiyo.