Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizindua club ya wanafunzi wa shule ya John Bosco kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya matembezi ya amani kwa ajili ya juma la mazingira kidunia yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya John Bosco iliyopo Wilayani Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya John Bosco mara baada tu ya kuzingua club ya wanafunzi kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Baba Paroko wa Parokia ya Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha Padri Beno Kikudo akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi kuhusiana na maadhimisho hayo ya wiki ya matembezi ya amani kwa ajili ya juma la mazingira kidunia.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi St. John Bosco wakati wa maadhimisho hayo kushoto kwake ambaye ameshika bango lililokuwa na ujumbe wa kampeni ya mazingira Padri wa parokia ya Tumbi Beno Kikudo baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa club ya mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameshika moja ya mti kwa ajili ya kujiandaa kuupanda wakati wa maadhimisho hayo ikiwa ni kumbukumbu kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Baba Paroko wa Parokia ya Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha Padri Beno Kikudo akiwa ameshika mche wa mti kwa ajili ya kuupanda wakati wa sherehe za maadhimisho hayo ya wiki ya matembezi ya amani yaliyofanyika mjini Kibaha.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi St. John Bosco iliyopo Wilayani Kibaha wakiwa katika maandamano maalumu ya matembezi ya amani huku wakiwa wamebeba mabongo amabyo yalikuwa yameandikwa ujumbe mbali mbali kuhusiana na juma la mazingira kidunia.
Wanafunzi mbali mbali wa shule ya St, John Bosco wakiwa katika maandamano maalumu kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya matembezi ya amani kwa ajili ya juma la mazingira kidunia amabapo kiwilaya yalifanyika katika shule St. John Bosco Wilayani Kibaha.
Muonekano wa baadhi ya wanafunzi wa shule ya St. John Bosco iliyopo mjini Kibaha wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya kuanza maandamano ya amani kwa ajili ya maadhimisho hayo.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………………………
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amekemea vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa baadhi ya wananchi kuamua kukata miti ovyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kupoteza uoto wa halisi na kusababisha baadhi ya maeneo kuwa majangwa na kuwataka pia kuachana na uchimbaji holela wa michanga pampja na uvuvi haramu.
Ndikilo aliyasema hayo Wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya wiki ya matembezi ya amani ya kikanisa kwa ajili ya juma la mazingira kidunia ambayo yamefanyika katika eneo la shule ya msingi ya St. John Bosco iliyopo Wilayani Kibaha na kuudhuliwa na viongozi mb ali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa dini.
Aidha Ndikiloa alisema kwamba uhifadhi wa mazingira ni suala la mtambuka hivyo ni muhimu kwa uhai wa viumbe pamoja na maendeleo ya uchumi wan chi hivyo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha anawajibuika katika suala zima la utunzaji wa mazingira pasipo kufanya mambo ambayo yatapelekea kuharibu mazingira.
“Kitu kikubwa ninachowaomba ni lazima tuhakikishe tunabadilika kwa kuweka misingi mizuri kuanzia ngazi za chini katika suala zima la utunzani wa mazingira na kuachana kabisa na vitendo vya ukataji wa miti ovyo pamoja na uchimbaji wa michanga hii ni hatari sana kwa hivyo mimi kama kiongozi wenu nina wasii kuachana na hali ni na badala yake pandeni miti kwa wingi,”alisema Ndikilo.
Pia Ndikilo alitoa wito kwa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda na kutunza mazingira kwa kuhakikisha kunakuwepo na mipango madhubuti kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya uchomaji wa mkaa pamoja na uchimbaji holela wa mchanga ambao unaleta madhara makubwa katika kuharibu mazingira kutokana na wakati mwingine kuendesha shughuli mbali mbali za kibinadamu.
Katika hatua nyingine Ndikilo alielezea madhara mbayo yanatajwa na wataalamu wa mazingira ni pamoja na kupungua kwa amaji safi, kuongezeka kwa magonjwa ya wanyama pamoja na mimea ikiwa sambamba na kutoweka kwa baadhi ya aina za wanyama mbali mbali.
Kwa upande wake Baba Paroko wa Parokia ya Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha Padri Beno Kikudo alisema kwamba wameamua kufanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na watoto wa shule ya St, John Bosco kwa lengo la kuwaelimisha juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira pamoja na kufanya uzinduzi rasmi wa klabu ya wanafunzi kwa ajili ya upandaji wa miti na kuitunzana kuilinda.
Kadhalika Kikudo alisema kwamba zoezi ambalo wamelifanya kw ajili ya maadhimisho hayo litaweza kuleta mabadiliko makubwa katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kwamba miti mbali mbali ambayo wameipanda wataitunza kwa lengo la kuweza kuboresha zaidi mazingira.
“Kikubwa kila mmoja wetu anao wajibu wa kutunza mazingira na kwamba ninawaomba wanafunzi ambao leo hii tumeweza kufanya uzinduzi kwa klabu maalumu ambayo itakuwa inasimamia masuala ya mazingira kuhakikisha kwamba wanailinda na kuitunza miti yote na kwamba kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake ili kusiwe na uharibufu wowote.
Naye mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi St. John Bosco ambaye amesoma sisala kwa niaba ya wenzake Ndigwako Mwakisisile amebaisha kwamba nia na madhimuni yao kupitia maaadhimisho hayo wataendelea kuhakikisha kwamba kuendelea kuhakikisha
Maadhimisho ya wiki ya matembezi ya Amani kwa ajili ya Juma la mazingira kidunia ambayo kimkoa yamefanyika katika shule ya St, John Bosco iliyopo Wilayani Kibaha yamepewa kauli mbinu isemayo “Jubilee ya Dunia yenye mwenendo mpya na tumaini jipya.