Kulia,Sunday Cuthbert Mratibu wa mashindano yaArusha innovation Summit, Katikati Pamela Chogo Msimamizi wa kituo cha kuendelea bunifu za biashara Chuo cha Uhasibu Arusha, Kushoto ni Happy Mdenye Mwenyekiti UNI Splash Show(Picha na Jane Edward, Arusha)
********************************
Jane Edward, Fullshangwe,Arusha
Chuo cha uhasibu Arusha kikishirikiana na taasisi mbalimbali kinatarajia kuanzisha mashindano ya ubunifu ya biashara kwa vijana lengo likiwa ni kuwainua vijana walioko mtaani na vyuoni kuweza kujiajiri
Mbali na chuo hiko kufahamika kutoa mafunzo katika fani ya Uhasibu lakini pia kimekuwa kikijihusisha na kuwajengea uwezo vijana mbalimbali kuweza kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali za kujipatia kipato na kuacha kuwa tegemezi.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa kituo cha kuendelea bunifu za biashara kutoka Chuo hicho cha Uhasibu Pamela Chogo,
anasema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuwasaidia vijana hususani walioko mavyuoni kuanza kutengeneza ajira binafsi
Amesema kuwa Vijana wengi wamekuwa wakilalamika ukosefu wa ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya Chuo na hivyo wakaona waje na mkakati mahususi wa kumkomboa kijana katika kufanya biashara bunifu.
Sunday Massawe ni mratibu wa mashindano haya ambayo yanajulikana kama Arusha Innovation summit anasema kwa pamoja yatatoa fursa kwa vijana katika kuonyesha uwezo wao katika kuinua vipaji vyao yakiwasaidia zaidi vijana katika kujiajiri
Hata hivyo ametoa Rai kwa vijana wote kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo ili kuweza kubadilishana uzoefu na wadau watakaoudhuria maonyesho hayo.
Ni mwaka wa pili sasa mashindano ya Arusha Innovation Summit yanafanyika ambapo kwa mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha vijana wengi zaidi huku yakidhaminiwa na taasisis mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Arusha