Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, ACP Ibrahim Mahumi akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, ACP Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya siku moja kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA),akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya siku moja kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, ACP Ibrahim Mahumi akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya siku moja kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, ACP Ibrahim Mahumi,ameziagiza Taasisi zote za Umma kuhakikisha zinatekeleza kikamilifu Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya Mwaka 2019 na Kanuni zake ambayo imetungwa kwa lengo la kusimamia matumizi ya Serikali Mtandao.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao .
ACP Mahumi amesema kuwa umakini katika suala zima la usalama mitandaoni na kwenye mifumo unahitajika ili kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha huduma kwa umma kwa njia ya Serikali Mtandao.
Aidha amesema kuwa kila Taasisi inalo jukumu la kuwaelimisha watumishi wake ili wawe na uelewa wa pamoja wa namna ya kutekeleza Sheria ya Serikali Mtandao pamoja na kanuni zake kwa lengo la kuepuka athari zitakazoweza kujitokeza kwa kutokuzingatia sheria hiyo.
“Watu wa TEHAMA kazi yenu kubwa ni kurahisisha utendaji kazi Serikalini hivyo, naamini mafunzo haya yatawasaidia kuhimiza utekelezaji wa Sheria ya Serikali Mtandao”amesema ACP Mahumi
Hata hivyo ACP Mahumi ameziasa Taasisi za Serikali ambazo zinasuasua kutumia Serikali Mtandao kuhakikisha zinatumia fursa ya uwepo wa Serikali Mtandao ili wananchi wanufaike na huduma.
Sheria ya Serikali Mtandao Namba 10 ya mwaka 2019 ilianza kutumika rasmi tarehe 15 Disemba, 2019 baada ya kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo iliiwezesha iliyokuwa Wakala ya Serikali Mtandao kuwa Mamlaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Dk Jabiri Bakari amesema mafunzo haya ya leo yatawapa uelewa kuhusu vifungu mbalimbali vya sheria hiyo na kanuni zake pamoja na mabadiliko yanayotokana na sheria hiyo ikiwemo kuibadili kutoka kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kuwa Mamlaka ya Serikali Mtandao pamoja na majukumu ya mamlaka hiyo.
” Niwasihi washiriki wote wa mafunzo kuzingatia kile kitakachotolewa leo lakini pia wakawe watumiaji wazuri wa Sheria hii maana wote tunajua sheria ni msumeno watakaokiuka watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni,” Amesema Dk Jabiri.