Home Uncategorized MATUKIO KATIKA PICHA UCHAGUZI WA ASKOFU MKUU KANISA LA E.A.G.T

MATUKIO KATIKA PICHA UCHAGUZI WA ASKOFU MKUU KANISA LA E.A.G.T

0

Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T aliyemaliza muda wake Dkt. Brown Abel Mwakipesile akitoa neno la shukran kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu walioshiriki katika uchaguzi wa Viongozi wa Kanisa hili ulifanyika tarehe 25 Septemba, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma, mkutano huo ulihudhuria wa wachungaji wa makanisa yote ya EAGT nchini.

Katibu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T aliyemaliza muda wake Dkt. Leonard Mwizarubi akitoa hotuba kuhusu kanisa hilo wakati wa uchaguzi huo mapema hii leo.

Baadhi ya wachungaji walioshiriki katika uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa kanisa la E.A.G.T wakifuatilia mkutano huo

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T Dkt. Brown Abel Mwakipesile (Wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Kanisa la E.A.G.T Dkt. Alphonce Mwanjala  (katikati) pamoja na Mch. la E.A.G.T Tabata Msimbazi Alexander Simbila wakati wa uchaguzi huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akitoa neno kwa wajumbe na viongozi walioshiriki katika uchaguzi huo uliofanyika leo Septemba 25, 2020 katika uchaguzi wa  viongozi wa Kanisa la E.A.G.T kwa ngazi ya Kitaifa.

Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T aliyemaliza muda wake Dkt. Brown Abel Mwakipesile (mwenye tai ya blue) pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Leonard Mwizarubi (kulia kwake) pamoja na aliyekuwa Mhazini Mkuu, wa kwanza kushoto Mch. Praygod Mgonja wakiimba wimbo wa kumwabudu Mungu wakati wa uchaguzi huo.

 (PICHA NA ALEX SONNA – FULLSHANGWE ,DODOMA)