Home Mchanganyiko WATAALAM WA TEHAMA KUSAJILIWA RASMI

WATAALAM WA TEHAMA KUSAJILIWA RASMI

0

Katibu Mkuu, Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Zainab Chaula,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu  kongamano la nne la mwaka la TEHAMA linalotarajia kufanyika kati ya Oktoba 7 hadi 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

……………………………………………………………………………….

Na Alex Sonna

WATAALAM wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), wanatarajiwa kuanza kusajiliwa rasmi katika kongamano la nne la mwaka linalotarajia kufanyika kati ya Oktoba 7 hadi 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu, Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk.Zainab Chaula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo.

Amesema hatua hiyo ni katika kutekeleza sera ya taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 inayotaka kuwa na nguvu kazi yenye maadili na uwezo wa hali ya juu katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na kukuza mchango wake katika maendeleo ya nchini.

“Kwa kipindi kirefu tumekuwa na wataalamu wanaosimamia miundombinu, huduma na mifumo yetu muhimu ya TEHAMA pasipo kutambulika uwezo na maadili yao, hivyo katika kongamano la mwaka huu, moja ya tukio muhimu ni kuzindua rasmi usajili wa wataalam wabobezi wa TEHAMA na waziri mwenye tamana ya TEHAMA atatoa vyeti vya usajili kwa wataalam 100,”amesema.

Aidha, Dk. Chaula amesema mijadala katika kongamano hilo lenye kaulimbiu ‘kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda: kinachofanyika, changamoto na fursa’.

Amesema matokeo ya mijadala katika kongamano ni kuwa na mkakati jumuishi wa Tanzania ya kidijitali utakaoongeza kasi ya maendeleo ya nchi katika kipindi hiki ambacho mifumo ya TEHAMA inatumika kwa kiwango kikubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii katika maisha ya kila siku.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sosthenes Kewe amesema ili Tanzania kufikia uchumi wa kidijitali kunaitajia kuendelea wa TEHAMA maeneo na katika huduma zote.

Amesema kwa upande wa huduma za kifedha, TEHAMA imesaidia sana kuongeza huduma za fedha na kusisita haja ya huduma hiyo kusambaa zaidi kufika katika maeneo mengi nchini.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA, Samson Mwela amesema mijadala katika kongamano hilo italenga ni kupitia dira ya dijitali Tanzania, fursa za dijitali na ilivyochangia uchumi, ujuzi, ubunifu na mapinduzi ya teknolojia na mifumo kuelekea dijitali.