****************************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Sept 24
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo, amewataka Vijana mwaka huu wavunje rekodi ya kujitokeza kwa wingi kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi CCM,katika uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Aidha mgombea huyo amesema kwamba ushuhuda wa kuwaomba wakipigie kura nyingi chama hicho kinaonekana wazi, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mgombea urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli aliyeleta maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali.
Alisema kuwa ukiachilia kazi kubwa iliyofanywa na Serikali inayoundwa na chama hicho kitaifa, mtangulizi wake Humoud Jumaa amefanyakazi nzuri katika nyanja za elimu, afya na nyinginezo jimboni humo, huku akisema kwa mwaka wa 2020/2025 chama kimemuona yeye ampokee Jumaa.
Amewaomba vijana kumng’arisha kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM, mafiga matatu kwa miaka mitano ijayo.
Mwakamo anasema,Jemedali wetu Dkt. John Magufuli anausemi wake anaousema kuwa wa-Tanzai wenzangu nipeni kura za kutosha nawaahidi sintowaangusha, nami naungana na usemi huo, jitokezeni kwa wingi Oktoba 28 tumpigie kura Dkt. Magufuli, Mimi Mwakamo pamoja na wagombea wote wa CCM,”
Nae mgombea Udiwani Kata ya Mlandizi Uephrasia Kadala aliwataka wana- Mlandizi kutofanya makosa, wajitokeze kwa wingi wawachague wagombea wote waliosimamishwa na chama hicho ili waendeleze kazi ambayo tayari imeshaanzishwa na waliotangulia.
Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa Remy Ludovick aliwaasa wakazi wa Kibaha Vijijini kuacha kusikiliza maneno wanayoambiwa na watu wasioitakia mema Jimbo hilo, badala yake wawapuuze, ikifika Oktoba 28 wakipigie kura za kutosha chama hicho.
Meneja wa Kampeni, Hassani Kazimoto alieleza ,katika uchaguzi ,wananchi wasiangaike kutafuta majina ya wagombea wa chama hicho, wa huenda yakaandikwa mbele nyuma, badala yake waangalie rangi ya njano na kijani.