Home Mchanganyiko MAADHIMISHO YA SIKU YA BAHARI DUNIANI KUFANYIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU

MAADHIMISHO YA SIKU YA BAHARI DUNIANI KUFANYIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU

0

Na Magreth Mbinga

Siku ya bahari duniani tunafanya maadhimisho kila mwaka siku za mwisho wa mwezi Septemba l lengo ni kuonesha umuhimu wa kuwepo kwa bahari na usafirishaji wa maji.

Hayo yamezungumzwa na Capteni Dilshad Murtaza katika maadhimisho ya siku ya bahari na kusema kuwa wao ni mabaharia pia wanaendesha na kutengeneza meli na wafanyakazi wa nchi kavu wanawapokea pindi watokapo baharini.

Aidha Murtaza amesema kuna mabaharia wengi wanawake wamewaacha nyuma kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao kwa kushindwa kurejesha upya vyeti vyao na wengine vipingamizi wanavyopata kutoka katika familia zao.

Pia Murtaza amesema wao kama mabaharia wa kike wanamfanya mwanamke aendelee asikate tamaa wanaweza kumtetea kwa hali moja au nyengine.

“Nilipoanza kazi ya ubaharia nilifanya katika mazingira magumu sana hasa wazazi wangu wahakuniunga mkono kwakuwa natoka familia ya sini sana na walisema kuwa kazi hiyo inafaa kwa wanaume tu”amesema Murtaza.