…………………………………………………………………..
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara, KMC FC, kesho watashuka dimbani kukutana na Kagera Suger mchezo utakaopigwa katika Dimba la Kaitaba Mkoani Kagera saa nane kamili mchana.
Hadi sasa kikosi hicho cha KMC FC ambacho kimeweka kambi Mkoani Kagera kipo kwenye uimara wakutosha na kwamba katika mchezo huo watahakikisha kuwa wanaondoka na ushindi wa alama tatu muhimu ambazo zitawawezesha kuendelea kusalia katika nafasi ya kwanza.
KMC FC inakwenda kucheza mchezo wake wa nne, lakini pia ni wapili ugenini na kwamba hadi sasa haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara Septemba 17 mwaka huu na hivyo kuiwezesha timu hiyo kuwa na alama tisa pamoja na magoli nane.
Hadi sasa KMC imeshacheza michezo yake ambayo ni dhidi ya Mbeya City, Tanzania Prisons , Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga.