Mratibu wa Shirika la SOS kutoka makao makuu
jijini Dar es salam Mpeli Karonge akiendelea kutoa elimu ya namna ambavyo mifumo bora inatakiwa kuwa katika kukabiliana na changamoto za ukatili
****************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Watetezi wa haki za wanawake na watoto wamesema iko haja kwa Serikali, taasisi mbalimblali na wananchi kujikita zaidi katika kuimarisha mifumo ya kijamii ya ulinzi na usalama ngazi za vijiji na kata ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi kundi hilo.
Wakati wa kikao maalum chini ya Asasi ya kiraia ya utetezi wa haki za watoto Wilayani Mufindi SOS washiriki walisema mifumo iliyopo licha ya kuleta mafanikio kwa kiasi lakini kulingana na mapungufu yaliyopo imeshindwa kukomesha changamoto hiyo hasa vitendo vya ubakaji na Ulawiti dhidi ya watoto
Akizungumza mara baada ya kikao hicho Rehema Kasigi ambaye ni mlemavu wa macho alisema kuwa kundi kubwa la wenye ulemavu limekuwa wahanga wa wa vitendo vya ukatili kutokana na watendaji wa ukatili huo kudhani jamii kulingana na ulemavu walio nao hawana uwezo wa kujitetea.
Kasigi alisema kuwa licha ya kushuhudia vitendo vya kikatili vilivyowahi kutendeka katika maeneo anayoishi inatokana na sababu mbalimbali ikiwepo mira potofu kutoka kwa baadhi ya wananchi wanafanya ukatili huo.
Aidha Kasigi alisema kuwa anaiomba serikali na wadau zikiwemo mamlka za kisheria kuliangalia kw jicho la ziada kundi hilo ili kulilinda na matukio hayo ya ukatili kwa kuwasaidia wanawake na watoto kwa ujumla
Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya wilaya ya mufindi Mkoani Iringa Sechelela Dagaa alisema kuwa hali ya ukatili bado ipo na wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanakomesha na kunguza matukio ya ukatili.
Mratibu wa Shirika la SOS kutoka makao makuu jijini Dar es salam alisema kuwa kulingana na hali ilivyo Watetezi wa haki za wanawake na watoto wanasema.muarobaini wa changamoto hii ni kuimarishwa zaidi kwa mifumo ya kuzuia ukatili
Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na vitendo vya ulatili dhidi ya wanawake na watoto na mwito zaidi ukitolewa kwa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu juu ya malezi bora ya watoto wao ikiwa ninpamoja na kujenga urafiki na watoto wao ili kuwapa uhuru watoto kujieleza pindi kunapokuwa na dalili za kutendewa ukatili.