………………………………………………….
Na John Walter-Babati
Mbunge anaesubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais John Pombe Magufuli haijawahi kuwasahau wananchi.
Ameyazungumza hayo jana Septemba 22,2020 kwenye kampeni za Kuomba kura za Chama cha Mapinduzi kwa Mbunge, Diwani na Rais, zilizofanyika katika Kijiji cha Nakwa na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James.
Gekul amewaambia wananchi kuwa Wema waliofanyiwa na Rais Magufuli katika Jimbo la Babati Mjini kwa kipindi cha miaka mitano, fadhila kubwa ni kumpigia kura pamoja na wabunge na maiwani ifikapo Oktoba 28,2020.
“Hakuna haja ya kukinyima kura chama cha Mapinduzi,tuna kila sababu ya kuipa kura Ccm tukamilishe yaliyobaki” alisema Gekul
Mbunge huyo amesema Kijiji cha Nakwa ni Kijiji cha faraja na Mfano katika maendeleo Jimbo la Babati Mjini kwa kuwa kwa nguvu zao wameweza kujenga shule ya Msingi na Sekondari ya Kisasa pamoja na ujenzi wa Zahanati.
Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais John Magufuli kijiji cha Nakwa kimepokea shilingi milioni 801 ambazo zimekamilisha Mradi wa maji ambao ulikwama kwa miaka Mingi na kwa sasa wananchi wanafurahia huduma ya maji.
Aidha amesema katika kunusuru wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shule, Serikali imesaidia kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nakwa na kupata usajili kamili ambapo awali ilikuwa kama shule shikizi ya Bagara Sekondari.
Gekul amesema pamoja na hayo serikali ya Rais Magufuli imetoa shilingi M/ilioni 152 kwa ajili ya Ujenzi wa Mabweni ya watoto wa kike ambao unaendelea kwa sasa.
Kijiji cha Nakwa kilichopo kata ya Bagara, kina wapiga kura zaidi ya elfu tatu 3000