…………………………………………………….
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara , KMC FC leo imeondoka Mkoani Shinyanga kuelekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kukabiliana na timu ya Kagera Suger mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kaitaba Septemba 25 saa nane kamili mchana.
Timu hiyo imeondoka kwa usafiri wa basi na itaweka kambi mara itakapofika na kwamba wachezaji watapumzika kabla ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo ambapo Kagera Suger ni wenyeji.
Katika kikosi hicho hakuna majeruhi na kwamba wote wanahali nzuri hivyo wako tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambapo Timu ya KMC FC inahitaji ushindi huo kwa ajili ya kuendeleza hari ya kupata matokeo mazuri na hivyo kusalia kwenye nafasi ya kwanza.
Jana KMC FC ilicheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Mwadui ambapo ilipata matokeo mazuri kwa kuifunga mabao mawili kwa moja na hivyo kurudi kweye nafasi ya kwanza.