Home Mchanganyiko NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE...

NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

0

******************************

Leo tarehe 21 Septemba, 2020 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Khamis ametembelea Banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji cha Bomba Mbili mjini Geita.

Mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam, ameelekeza Tume ya Madini kujipanga zaidi katika maandalizi ya Maonesho ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Oktoba, 2021 Dubai.