Home Mchanganyiko ENDAPO TUTATUMIA RASILIAMALI ZETU TULIZONAZO ITARAHISISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO-PROF.MCHOME

ENDAPO TUTATUMIA RASILIAMALI ZETU TULIZONAZO ITARAHISISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO-PROF.MCHOME

0

Baadhi ya wadau wa Mkutano kujadili umuhimu wa ulinzi na Utajiri na Maliasili wakifatilia baadhi ya mada zilizotolewa katika Mkutano huo(Picha na Jane Edward, Arusha)

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Sifuni Mchome akifungua Mkutano uliojumuisha Makatibu wakuu na wakuu wa Serikali, katika kujadili umuhimu wa ulinzi na Utajiri na Maliasili(Picha na Jane Edward, Arusha)

Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Christine Musisi akizungumza na Wadau wa Mkutano huo jijini Arusha(Picha na Jane Edward, Arusha)

***********************************

Na Jane Edward,Fullshangwe Arusha

Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria ,Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa,endapo nchi yetu itazitumia rasilimali tulizonazo itasaidia sana kuharakisha shughuli za maendeleo Kama zilivyo kwa nchi zingine ambazo uchumi wao umeweza kukua kutokana na matumizi mazuri ya rasilimali hizo.

Profesa Mchome alisema kuwa,endapo nchi yetu itazitumia asilia zilizopo vizuri tunaweza kupata maendeleo ambayo tunahitaji katika nchi yetu .

Alisema kuwa, katika nchi yetu kuna ukuaji mzuri wa mapato katika sekta ya madini na mazao kwa ujumla ,na hizo sekta zikiendelea kukua katika uzalishaji na katika maeneo mbalimbali nchi itapata kipato cha kutosha na kuleta maendelea ya kutosha katika tasnia mbalimbali.

Profesa Mchome aliongeza kuwa,utajiri asilia na maliasilia tulizonazo zinatakiwa zitumike kwa manufaa ya nchi na watu wake na sio kwa manufaa ya nchi za nje.

Profesa aliyasema hayo katika kikao cha makatibu wakuu na wakuu na Taasisi za serikali ambao wamekutana kujadili mfumo jumuishi wa uangalizi wa utajiri na maliasilia za nchi.

Naye Mhadhiri mwandamizi wa uchumi chuo kikuu Cha Dar es Saalam (UDSM),Dokta Abel Kinyondo alisema kuwa,Kuna njia mbili za kuhakikisha wananchi wananufaika zile Kodi na tozo mbalimbali zinazotokana na maliasili zetu serikali inazitumia kwa namna ya kimkakati kuwarudishia wale walioko chini kabisa waweze kunufaika nazo.

Dokta Kinyondo alisema kuwa ,lazima tujue kuwa wenye kufaidika zaidi na hela sio kwenye tozo na Kodi bali wananchi waunganishwe moja kwa moja katika mnyororo wa thamani kwani sehemu kubwa ya mapato zinazotokana na rasilimali zinatumika katika matumizi.

Alisema kuwa,ni wajibu wetu kuhakikisha tunajipanga na kuangalia vizuri kuhakikisha wananchi wananufaika kwa namna moja ama nyingine lazima washirikishwe katika mnyororo wa thamani katika maliasili hizo.

Mwakilishi mkaazi wa UNDP ,Christine Musisi ambao ndio waandaaji wa mkutano huo,alisema kuwa,mkutano huo ni muhimu Sana kwani wanaangalia namna maliasili za nchi yetu zitakavyoweza kuwanufaisha watanzania wenyewe kwani Tanzania Kuna fursa nyingi Sana ambazo zikitumiwa vizuri zitaleta manufaa na maendeleo makubwa .