Mgombea wa udiwani katika kata ya Nduli kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Leonce Marto akiomba kura kutoka kwa wananchi wa kata Nduli walipojitokeza kwenye ufunguzi wa kampeni ya jimbo la Iringa Mjini.
*********************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mgombea wa udiwani katika kata ya Nduli kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Leonce Marto amevitaja vipaumbele vyake14 vya kimaendeleo katika kata hiyo ikiwepo tatizo la migogoro ya ardhi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni kuwania udiwani wa kata ya Nduli alisema kuwa wananchi wa kata hiyo wanakabiliwa na tatizo la mtandao wa maji kwenye mitaa hivyo akipewa ridhaa na wananchi wa kata hiyo atahakikisha anatatua kero hiyo.
Alisema kuwa ilishughuli za kimaendeleo ziendelea kwa wananchi bila mkwamo wowote ule ni lazima tatizo la maji litatuliwe kwa wakati ili kupisha shughuli nyingine za kimaendeleo ziendelee.
Marto alisema kuwa kata hiyo inakabiliwa na migogoro mingi ya Ardhi kutokana na uwepo wa viongozi ambao hawasimamii vizuri mipango bora ya matumizi ya ardhi hivyo kuanzisha migogoro mingi.
“Nikipewa ridhaa ya kuwa diwani hii ya Nduli nitahakikisha natoelimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya ardhi,auzaji na ununuaji wa ardhi kuepuka dhuruma ambayo inasababisha migogoro hiyo”alisema Marto
Alisema kuwa atahakikisha anatatua na kuboresha sekta ya elimu kuanzia miundombinu ya majengo na kutoa bonanzi kwa walimu na wanafunzi shule za msingi ili kuboresha ufaulu na utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi.
Aidha Marto alisema kuwa kata hiyo bado inategemea kilimo kwa asilimia kubwa hivyo ni lazima kuhakikisha wakulima wanalima kilimo cha kisasa na chenye faida kwa wakulima hao ilikiwa sambamba na kuboresha miundombinu ya barabara kwa lengo la kurahisisha usafiri.
Marto alisema kuwa swala la michezo,mikopo,huduma ya afya,masoko,wazee,yatima,wananchi wasio wenye uwezo yaani masikini,kuboresha mawasiliano ya simu kwa wananchi wa kata hiyo hivyo vyote vitaboreshwa ili kuchochea maendeleo ya wananchi wa kata ya Nduli