******************************
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoa wa Arusha,bw Ambroce Malai amesema kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo ana uwezo mkubwa sana wa kuleta maendeleo hivyo basi wanachama wa Ccm pamoja na wananchi wa jimbo la Arusha mjini wanatakiwa kumpa kura za kishindo
Aidha alisema kuwa kwa kipindi ambacho bw Gambo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Arusha aliweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya afya ambapo aliongeza idadi ya vituo vya afya lakini hata hospitali za wilaya
Aliyasema hayo juzi kwenye uzinduzi wa kampeni za udiwani katika kata ya sinoni ambapo alidai kuwa wakazi wa jimbo la arusha mjini hawatakiwi kukosea kabisa
Alifafanua kuwa mgombea huyo anatosha kabisa katika nafasi hiyo kwa kuwa tayati alishaonesha uwezo mkubwa sana wa kuokoa na kutatua changamoto ambazo zipo kwenye jamii ambayo inawazunguka
Alidai kuwa mbali na wakazi wa jimbo la arusha mjini kutoa kura zao kwa bw Gambo pia wanatakiwa kutoa kura za ndio tena kwa madiwani lakini pia hata kwa Raisi Magufuli ambaye naye amefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta na nyanja mbalimbali hapa Tanzania
“Nawasihi sana watanzania wasikosee kura zote za ndio kwa madiwani wetu wa ccm,wabunge na hata Raisi haitapendeza hata mmoja kukosa nafasi yake na endapp kama watakuwa wote ni raisi maendeleo kuwepo kwa kasi sana tofauti na unapokuwepo upinzani” aliongeza
Alihitimisha kwa kusema kuwa ni vema sasa kwa kila mtanzania kujiyokeza siku ya kwends kupiga kura na kuwachagua wagombea wa ccm ili waweze kuharakisha maendeleo
Naye mgombea udiwani wa kata hiyo ya Sinoni Bw Michael kivuyo alisema kuwa kata hiyo ni moja ya kata ambazi bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo tu mara atakapochaguliwa ataweza kwenda kuzitatua
Alidai kuwa kwa wakatk hui sasa ni muda muafaka kwa watanzania hususani wakazi wa kata hiyo ya Sinoni kuweza kupata mafanikio kupitia wagombea ambao watateuliwa na wananchi kuanzia ngazi ya udiwani hadi Raisi