*************************************
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dkt. Tulia Ackson ameshiriki katika kampeni za kunadi sera za chama hicho katika kata ya Iyunga iliyopo jijini humo kuelekea uchaguzi mkuu wa October 28, 2020 ambapo amewataka Wananchi kuchagua viongozi wanaojitoa kwa ajili ya manufaa ya wengi na sio wanaotaka kujinufaisha wenyewe na matumbo yao.
“Wana-Mbeya chagueni Mbunge anayejiongeza na sio kulalamika kila mara, tunaposema tutafanya mambo hapa tunamaanisha na tayari mmeona ni mambo mangapi kabla hamjanipa kura nimekwishayafanya ndani ya Jiji hili”- Dr. Tulia Ackson
“Sitaweza kuyamaliza na nitasema kwa ushahidi, nimeboresha miundombinu ya elimu katika shule nyingi hapa jijini, Afya, Ukarabati wa barabara za mitaani licha ya kwamba bado miundombinu ya barabara ni mibovu sasa nipeni kura za kutosha niwaoneshe maajabu”- Dr. Tulia Ackson
“Ndugu zangu chagueni viongozi wenye Connection, sasa asije hapa mtu akakudanganya kwamba haya ni maendeleo ya vitu. Maendeleo ya mtu tunapima kwa vitu alivyonavyo na sisi watu wa Mbeya tutapimwa kwa maendeleo ya miundombinu mizuri tutakayokuwa nayo baada ya kuichagua CCM”- Tulia Ackson.