Home Mchanganyiko WAMACHINGA JIJINI DODOMA  WATOA PONGEZI  KWA  RAIS MAGUFULI KWA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

WAMACHINGA JIJINI DODOMA  WATOA PONGEZI  KWA  RAIS MAGUFULI KWA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

0

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga akizungumza na wandishi wa habari na machinga ambao waliojitokeza katika ofisi za chama hicho kutoa tamko la Kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuwajali machinga tukio hilo limefanyika leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wamachinga wakimsiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga alipokuwa akiwapongeza wamachinga waliofika ofisi kwake kutoa tamko la Kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuwajali machinga tukio hilo limefanyika leo jijini Dodoma.

Mwenyekiti Msaidizi wa machinga Bw.Bruna Mponzi,akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakitoa pongezi Rais Dk John Magufuli kwa kuwajali machinga tukio hilo limefanyika leo jijini Dodoma.

Mweka Hazina wa Machinga Athuman Ally,akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakitoa pongezi Rais Dk John Magufuli kwa kuwajali machinga tukio hilo limefanyika leo jijini Dodoma.

Mjasiliamali  Bi.Lionatha Msakafu,akitoa pongezi kubwa kuhusu mambo makubwa waliyofanyiwa na Dk John Magufuli ya kimaendeleo leo jijini Dodoma.

Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Henry Mwenge akipokea salamu za wamachinga wa mkoa huo walizozitoa kwa Mgombea Urais wa CCM na Rais Dk John Magufuli kwa kuwafanyia maendeleo wamachinga wa mkoa huo.

Mwenyekiti wa Machinga Soko la Sabasaba Elizabeth Siame akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu mambo makubwa waliyofanyiwa na Dk John Magufuli ya kimaendeleo.

………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAJASIRIAMALI wadogowadogo Jijini Dodoma (Wamachinga) wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt  Magufuli kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zote zilizokuwa zikiwakumba hapo awali.
Wakitoa Tamko hilo leo jijini Dodoma  katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dodoma Mwenyekiti Msaidizi wa machinga Bw.Bruna Mponzi  amesema kuwa wameona ni vyema kurudisha fadhila kwa serikali kwa kila kitu walichofanyiwa kwani kazi zao kwa sasa wamekuwa wakifanya kwa uhuru mkubwa tofauti na hapo awali.
‘’ Kwa upande wetu mmekuwa watetezi wetu wa nguvu kwa sababu ni tofauti na awamu nyingine zilizopita tulikuwa tunaishi kwa shida na hofu kwenye maeneo yetu ya kazi lakini sasa tunaishi kwa uhuru mkubwa Zaidi’’ Amesema Mponzi.
Naye Mweka Hazina wa Machinga Athuman Ally amesema wametafuta fursa hiyo kwa muda mrefu ya kumshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa yale ambayo amewafanyia wamachinga katika jiji la Dodoma.
‘’ Mpaka sasa hivi tuna imani na Mh. Rais kwamba anaweza na ataendelea kutenda juu ya machinga zaidi ya hayo na anaweza kutoa tamko jingine zuri juu ya uhuru wa wamachinga”Amesema
Katibu wa Wamachinga Stendi ya Mabasi Dodoma Shaban Suleiman Kisamvu amesema, ‘’nimesimama hapa kuwakilisha salamu za wamachinga wa stendi ya mabasi wanamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuweka stendi hiyo ambayo imekuwa ni ya kisasa zaidi’’ Amesema
 Mwenyekiti wa Wamachinga Soko la Sabasaba Bi.Elizabeth Siame amesema anamshukukuru kwa kila kitu kwani kazi zao sasa zimekuwa zikifanyika kwa uhuru mkubwa huku Leonatha Ernest Msakafu amesema kwa kipindi cha nyuma wajasiriamali wadogo walikuwa wakihangaishwa ,wakinyanyasika lakini kwa sasa hawakumbani na changamoto yoyote ile.
Kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma,Pili Mbanga   amewashukuru wamachinga wote mkoani hapa kwa kuthamini kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli .
‘’ kwakweli nyinyi wamachinga ni watu wema sana mmetambua fadhila alizowafanyia Rais Magufuli na ujumbe huu utafika kwa Mh. Rais ”Amesema Pili.
Katibu Mwezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Henry Msunga Mwengi amesema wamachinga ni sehemu ya watanzania wanahaki kama watu wengine na wanastahili heshima.
‘’Kwa yote yalifanyika kwa sasa wamachinga wanapata heshima mno unajua kwanini kwasababu leo mmachinga anaheshimika leo machinga anaona fahari kwa kazi anayoifanya kwa kujitambulisha kuwa ni machinga.’’Amesema