MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akikagua gwaride kwa wahitimu wa mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
Wahitimu wa mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora wakitoa heshima kwa mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akihitimisha mafunzo hayo leo jijini Dodoma.
Wahitimu wa mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora wakila kiapo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Meja Jenerali Charles Mbuge (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo hayo leo jijini Dodoma.
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akitoa zawadi kwa wahitimu watatu wa mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati waliofanya vizuri katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
Akisoma risala ya wahitimu hao, Nenelwa Mwihambi
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akipokea risala ya wahitimu hao kutoka kwa Nenelwa Mwihambi wakati wa kuhitimisha mafunzo akikagua ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT, Kanali Amos Mollo,akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kikosi JKT Makutupora, Luteni Kanali Festo Mbanga,akitoa taarifa fupi ya mafunzo hayo yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge,akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu mara baada ya kufunga mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati katika Kikosi cha JKT Makutupora yaliyohitimishwa leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge amefunga mafunzo ya vijana 41 ambao ni watumishi wa Bunge yaliyopewa jina la Operesheni Uchumi wa Kati, huku akiwataka kutanguliza mbele maslahi ya Taifa kwenye majukumu yao.
Akifunga leo mafunzo hayo katika Kikosi cha JKT Makutupora, Meja Mbuge amesema wahitimu hao wanapaswa kutumia mafunzo waliyopata kwa kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuzingatia kiapo kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Amewataka kuwa viongozi bora na mfano wa kuigwa kwa wengine ili kuonesha kuwa mafunzo waliyopata yana tija kubwa kwa Taifa.
“Mafunzo haya yalianza Agosti 17 mwaka huu hadi leo, mmeonesha namna mlivyo na uzalendo kwa nchi yenu kwani tangu mmeingia hakuna aliyetoroka na kusema hapendi mafunzo haya,”amesema.
Amewataka kuwa tayari muda wote kulitumikia Taifa kwa kazi mbalimbali kwa kuwa wamefundishwa ukakamavu, uzalendo na uhodari.
“Kupiti mafunzo mliyopata nina imani mpo tayari kutumikia Taifa na kulinda Taifa, mmefahamu dhana ya uzalendo, umoja, mshikamano, ukakamavu na kujiamini, mnapaswa mkatumie kutatua changamoto kwenye maeneo yenu ya kazi, changamoto huzaa fursa,”amesema.
Amesema ni jukumu lao kubadili mitazamo hasi kwa watumishi wa umma na jamii ambao hawakupata fursa juu ya umuhimu wa mafunzo hayo.
“Niwasihi yale yote mliyopata ya uaminifu mliyoonesha kwa Taifa, mkayaendeleze wakati wote wa utumishi wenu, nyie ni kati ya watumishi wachache mliokula kiapo cha uaminifu na utiifu, muwe viongozi bora, kiongozi siku zote hasimamiwi, anapanga mipango ya kazi,”alisema.
Ameongeza “Jeshi litaendelea kuwatumia kwa kuwa ninyi ni jeshi la akiba na mmejifunza mbinu mbalimbali za kivita,ninachowaomba kuanzia sasa muwe tayari kutumikia nchi yetu wakati wowote na sehemu yoyote kwa maslahi ya nchi na si ya watu wengine.”
Kuhusu uchaguzi mkuu 2020, Kiongozi huyo amewataka watanzania kusikiliza sera za wagombea na kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya Taifa na si ambao watadumaza maendeleo ya Taifa yaliyopatikana.
Awali, akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Kikosi JKT Makutupora, Luteni Kanali Festo Mbanga, amesema katika mafunzo hayo kulikuwa na wanawake 21 na wanaume 20 ambao wana umri kati ya miaka 22-55 na ni watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi.
Amesema walikuwa wepesi wa kuelewa mafunzo kwa nadharia na vitendo na kufikia viwango vizuri na wamefundishwa utunzaji na utumiaji wa silaha ndogondogo, kwata, mbinu za kivita, ujanja wa porini,uraia na uzalendo, usalama na utambuzi, uchimbaji wa mahandaki.
“Wamefundishwa na wakufunzi wanne mahiri, kozi imewajenga na kuwaimarisha kimwili wahitimu wetu, na masomo yamewafundisha kuwa na nidhamu na utii kwenye utendaji wa Bunge,”amesema.
Naye, Kaimu Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT, Kanali Amos Mollo, amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi kwa watumishi wengine.