RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Prof.Ratlan Paradede alipowasili katika Kiwanda Kipya cha Kukamulia Majani Makavu ya Mkarafuu Mgelema, wakati wa hafla ya ufunguzi wa kiwanda hicho leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiondoa kipazia kukifungua Kiwanda Kipya cha Kukamulia Majani Makavu ya Mkarafuu Mgelema Wilaya ya Chakechake Pemba, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salim Ali na (kulia kwa Rais) Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe.Prof.Dr.Ratlan Pardede na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe,
Haasan Hafidh
RAIS wa Zanziubar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akipongezana na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe.Prof.Dr. Ratlan Pardede baada ya kuondoa kipazia kuweka jiwe la msingi la Kiwanda Kipya cha Kukamulia Majani Makavu ya Mkarafuu kilichoko Mgelema Wilaya ya Wete Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Afisa Maabara wa ZSTC Pemba Ndg.Ali Amour Hamad, baada ya kukifungua Kiwanda Kipya cha Kukamulia Majani Makavu ya Mkarafuu Mgelema Wilaya ya Mkoani Pemba
WASANII kutoka Indonesia wakitowa burudani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kiwanda Kipya cha Kukamulia Majani Makavu ya Mkarafuu Mgelema Wilaya ya Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu)