Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kushoto) akizungumza mara baada ya kuingia makubaliano ya miaka mitatu ya kuendeleza wachezaji, makocha na waamuzi na waendeshaji wa Ligi yaHispania, La Liga San Tander. Kulia ni mwakilishi wa Alvaro Paya ambaye ni mwakilishi wa La Liga Tanzania.
Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kushoto) akipongezana na mwakilishi wa La Liga San Tander Tanzania, Alvaro Paya mara baada ya kuingia makubaliano ya miaka mitatu ya kuendeleza wachezaji, makocha na waamuzi na waendeshaji wa Ligi yaHispania, La Liga San Tander. Kulia ni mwakilishi wa Alvaro Paya ambaye ni mwakilishi wa La Liga Tanzania.
…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Mbet na waendeshaji wa ligi ya Hispania La Liga San Tander wameingia makubaliano ya kuendeleza vipaji nchini Tanzania.
Kampuni hizo mbili zimesaini mkataba wa miaka mitatu ambapo mbali ya kuendesha mafunzo ya soka kwa vijana, pia watafanya mafunzo kwa makocha na waamuzi kutumia wataalam wa La Liga.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba, Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa timu wanaoyoidhamini, KMC ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, nayo itafaidika na makubaliano hayo ambayo lengo lake kubwa ni kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Mushi alisema kuwa safari ya M-bet ya kukuza soka landani ya ilianza miaka miwili iliyopita na sasa wameamua kutanua wigo kwa kwenda kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
“Lengo hapa ni kuwapa faida wateja wetu ambao ndiyo nguzo pekee katika maendeleo ya kampuni yetu, mara baada ya ligi ya Hispania kumaliza kuruhusu watazamani na mipaka kufunguliwa, wateja wetu wataweza kubashiri na washindi watakwenda kuangalia ligi hiyo ya Hispania,” alisema Mushi.
Alisema kuwa ushirikiano huo wataweza kukuza vipaji na kutimiza ndoto za vijana ambao ndiyo nguzo kubwa ya maendeleo ya soka nchini,” alisema Mushi.
Mwakilishi wa La Liga San Tander wa Tanzania, Alvaro Paya alisema kuwa wamefurahi kuingia makubaliano na M-Bet na kuwa washirika wa pili baada ya klabu ya Yanga kuingia nayo makubaliano.
Paya alisema kuwa lengo la La Liga ni kuhakikisha mpira wa Tanzania unasonga mbele kwani wamegundua kuna vijana wengi wenye nia ya kuendeleza vipaji vyao, lakini wanakosa njia ya kufikia kwenye ndoto zao.