………………………………………………………………………………
Na Pius Ntiga, Arusha
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Mussa Matoroka, amesema chama hicho mwaka huu kimejipanga kumstaafisha rasmi kisiasa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema na badala yake aanze kufungasha virago kabla ya Oktoba 28 mwaka huu.
Matoroka ametoa kauli hiyo leo Mjini Arusha wakati wa mahojiano na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM inayolenga pia kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura OKTOBA 28 mwaka huu.
Aidha katibu huyo wa CCM amesema hali ya kisiasa Mkoani Arusha hivi Sasa Ni nzuri na Mkoa huo unajumla ya majimbo Saba na wana uhakika majimbo hayo yote CCM itashinda mwaka huu.
Amesema Arusha imebadilika na sio arusha ya miaka kadhaa iliyopita, hiyo yote inatokana na maguzi makubwa yaliyofanywa na Rais John Magufuli, licha ya kwamba Jimbo la Arusha Mjini kuwa katika upinzani kwa miaka iliyopita.
Kuhusu Leo kufungashiwa virago kauli ya Matoroka iliyoungwa Mkono wa wananchi ambao wamesema Miradi mikubwa ya kimkakati iliyoletwa na Rais Magufuli na watakachokifanya mwaka huu Ni kumpa zawadi Rais Magufuli kwa kumpigia Kura yeye pamoja na wagombea Ubunge na Udiwani wanaotokana na CCM.
Miradi hiyo imetajwa kuwa Ni pamoja na ule wa Maji Safi na Salama uliogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 500 uliopo eneo la Ngaramtoni.
Mradi huo Mkubwa wa Maji wa Arusha inatajwa kuwa umesaidia kuondoa kero ya maji kwa Arusha na mradi wa barabara wa bypass umesaidia pia kuondoa msongamano wa magari, hivyo wananchi wamepongeza.
Aidha, amesema Ujenzi wa Hospitali za wilaya na vituo vya Afya na elimu bure umechochea kazi ya maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Pia Barabara za vijijini Sasa zinapitika kwa urahisi hususani kule Ngorongoro tangu Uhuru upatikane mwaka 1961 mji huo ulikuwa haijawahi kuwa na barabara ya lami ambapo Sasa Kuna barabara ya lami na changarawe na zinapitika wakati wote.
Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri za wilaya nayo intajwa nayo kuwa ni Chachu ya wananchi kuendelea kuikubali CCM hasa katika miaka mitano iliyopita chini ya Rais Magufuli.
Pia ujio wa Treni ya mzigo na Abiria wananchi wa Arusha wamepongeza, kwani bidhaa Sasa zimeshuka Bei ikiwemo nauli za Treni ambazo Sasa zitasababisha nauli za mabasi kupunguza kwani watu watahamia kutumia usafiri wa Treni ya Abiria.
“Zawadi pekee ya kumpatia mwaka huu Rais Magufuli Ni kumpa Kura nyingi za ndio ili kurudisha heshima ya jiji la Arusha”. alisema
“Mikakati ya jumla ni kuwafikia wananchi wote kuwaomba kura na kuwaeleza Nini serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanya na kazi ya Chama katika Uchaguzi Ni kushika Dola”.
Kuhusu idadi ya wananchi walijiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura amesema ni jumla ya Milioni moja kaki tano na elfu hamsini, hivyo kwa idadi hiyo chama kinajivunia kuwa miongoni mwa wananchi hapo idadi kuwa ni wanaccm ambo wanaiunga Mkono serikali iliyopo madarakani.
Aidha Matoloka amewaomba wananchi wasibweteke na badala yake wajitokeze kwa wingi siku ya Jumatano ya mwezi wa kumi tarehe 28 wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na wakaipigie CCM kura za ndio kwa wagombea wake.
Wakati huo huo, wananchi wanofanya Biashara zao katika Soko Kuu ya Arusha wakiongozwa na Mgombea Udiwani wa kata ya Mjini Kati AbdulMasoud Tojo, wamesema mwaka huu hawatafanya makosa na watawachagua wagombea wote wa CCM akiwemo Mgombea Ubunge Arusha Mjini kupitia CCM Mrisho Gambo, licha ya mji wa Arusha kuwa ngome ya Upinzani.