*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege Fc inayoshiriki ligi kuu visiwani Zanzibar na kufanikiwa kuichapa mabao 2:0 katika uwanja wa Chamanzi.
Goli la kwanza lilifungwa na Mshambuliaji Waziri Jr mnamo dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati na bao la pili lilifungwa na kiungo wa kati wa klabu hiyo Mukoko ambaye aliuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Mlandege na kuzaa bao.
Yanga wataanza safari yao hapo kesho kwenda Mkoani Kagerakwaajili ya mechi yao ya ligi dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi.