KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wadau wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,(hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Bw.William Erio,akitoa taarifa ya mrejesho kutoka taasisi zinazotumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mhandisi Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa wasilisho la Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw.Alexander Sanga,akielezea mrejesho kutoka taasisi zinazotumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mhasibu Mkuu kutoka Taasisi ya Wakala wa Huduma ya Hifadhi za Msitu Tanzania,Peter Mwakosya,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mchambuzi wa Sera kutoka TARURA Dk.Noel Komba,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mhasibu Mwandamizi ,Edward Michael kwa niamba ya Mkurugenzi Mtendaji Benjamini Mkapa Hospital ,akizungumza kwenye Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) iliyofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inatarajia kuanza kutoa elimu ya matumizi ya malipo ya Serikali kwa njia ya Mtandao GePG kwa wananchi ili kuongeza uelewa kwa jamii juu ya matumizi ya mfumo huo mpya ambao umeleta mafanikio katika kukusanya mapato ya Serikali.
July 2017 Serikali ilizindua rasmi mfumo wa malipo ya makusanyo ya serikali kwa njia ya mtandao Government Electronic Payment Gateway GePG ambapo makusanyo yote ya Halmashauri na Taasisi za kiserikali hutumia kukusanya mapato yake.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James wakati wa Mkutano wa kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kiserikali (GePG) amesema kuwa mfumo huo umekuwa na mafanikio katika kukusanya mapato.
Bw.Jamese amesema kuwa mfumo huo bado umekuwa changamoto kwa wananchi hasa uelewa Kati ya GePG na Control number wengi wamekuwa wanashindwa kutofautisha.
” Wananchi wengi wanatumia mfumo huu na unawasaidia lakini wengi hawaelewi maana ya GePG na Control number wengi wanasema nimetuma kwa kutumia Control number tutapita maeneo mbalimbali kutoa elimu hiyo wajue” amesema Dotto James.
Hata hivyo amesema kuwa mfumo huo umerahisisha kazi katika maeneo mbali mbali ambapo umesaidia kuondoa changamoto nyingi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na mfumo huo Sasa unatumiwa na taasisi zaidi ya mia sita (600).
Amebainisha kuwa tangu kuanza kwa mfumo huo ukusanyaji wa mapato ya Serikali umeimarika Sana hadi kufikia asilimia 250 na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.
” Kabla ya mfumo huo tulikuwa tunakusanya bilioni 688 lakini kwa Sasa baada ya kuanza kwa mfumo huu tumefikia tilioni 2.6″ amesema.
Aidha ameonya kwa taasisi na halmashauri zote hapa nchini kutoanzisha mfumo wowote bila idhini ya Waziri wa Fedha na Mipango ili kudhibiti uanzishwaji wa mifumo kiholela.
Amesema Wizara imeweza kutengeneza mifumo minne katika Kudhibiti mapato ya Serikali na imeanzisha GePG, mfumo wa usimamizi wa matumizi ya Serikali MUSE, Mfumo wa usimamizi wa miradi ya maendeleo (kanzi data ya miradi ya maendeleo) na mfumo wa usimamizi wa misamaha ya kodi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Awali Mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu Cha Dar es saalam (UDSM),Prof.Dkt Joel Mtebe, amesema kuwa wamefanya utafiti kuhusu mfumo huo na kubainisha kuwa umekuwa msaada na kuwezesha ukusanyaji mzuri wa mapato ya Serikali.
“Tumepita maeneo mengi tumeona imekuwa msaada mkubwa na umedhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kuwawezesha watumishi katika maeneo yao kufanya kazi kwa wakati” amesema Dkt Mtebe.