Tarehe 11 September 2020 – Washindi wawili wa tuzo za mwaka 2020 za GoGettaz Agripreneur wametangazwa katika kongamono la Africa Green Revolution Forum Virtual Summit nchini Rwanda: Moses Katala Mwasisi Mwenza na CEO wa Magofarm Limited (Tanzania) na Daniella Kwayu Mwasisi Mwenza na CEO wa Phema Agri (Tanzania). Kila mshindi atapokea dola US$50,000 kwaajili ya kusaidia na kupanua uendeshaji wa biashara yao ya kilimo. Kama sehemu ya Generation Africa youth initiative, lengo la tuzo hii ni kuwaibua na kuwahamasisha vijana barani Afrika kukamata fursa katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo cha chakula wenye thamani ya $1Tn barani ndani ya miongo michache ijayo.
Wajasiriamali wengine wanne vile vile walitajwa kupokea tuzo ya $2,500 ya athari (Impact Award) Elizabeth Gikebe, Mwasisi na CEO wa Mhogo Foods (Kenya), Millicent Agidipo, Mwasisi mwenza na Meneja Uzalishaji wa Achiever Foods (Ghana), Dysmus Kisulu, Mwasisi mwenza na CEO wa Solar Freeze (Kenya) na Paul Matovu,Mwasisi na CEO wa Vertical Farm and Micro-Gardening (Uganda). Wajasiriamali hawa walichaguliwa na majaji kwa kuonyesha athari chanya katika mazingira au kwa jamii wanazotokana na biashara zao, kila mmoja akiwa anajitahidi kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu na kunufaisha jamii zao. Wajasiriamali wote 12 walioingia fainali na watapata ushauri, kuunganishwa na programu pamoja na kupata miongozo ya kuendelea na safari yao ya ujasiriamali.
Mashindano ya pili ya mwaka 2020 ya tuzo ya GoGettaz Agripreneur Prize yaliaanza mwezi Aprili na kwisha mwezi Juni mwaka huu. Zaidi ya waombaji 3000 wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 kutoka katika nchi 29 wamejiandikisha kushindana. Japo kuwa utofauti wao umeshika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo cha chakula kutokea katika uzalishaji wa msingi mpaka katika uvumbuzi wa teknolojia za kidigitali, Vijana wote sita wa kike na vijana sita wa kiume ni wajasiriamali kutoka katika nchi tisa za kiafrika ambao wamefanikiwa kuingia katika 12 Bora walikuwa wanafanana japo katika kitu kimoja: waliona tatizo na kufanya mipango mikubwa kutatua changamoto hizo kwa kuanzisha kampuni mpya katika sekta ya kilimo cha chakula Afrika.
Wajasiriamali na miradi iliyoingia fainali ya 12 Bora mwaka huu wanatokea Ghana, Kenya, Malawi, Morocco, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, Afrika ya Kusini, Tanzania na Uganda.
Katika shindano la kunadi wazo wakati wa fainali mapema wiki hii washiriki wote walioko fainali waliwasilisha mawazo yao moja kwa moja kupitia mtandao kwa dakika tatu mbele ya majaji nane ambao walikuwa na dakika mbili za kuuliza maswali. Hiki hapa ndio kiungo (Link) kukuwezesha kutazama shindano la kunadi wazo ambalo lilikuwa linatangazwa ulimwenguni kote katika mkutano wa AGRF na katika mitandao ya kijamii tarehe 8 Sept 2020. https://www.facebook.com/GoGettazAfrica/videos/645057906424901
Kwa mwaka huu majaji 8 (tazama hapa chini) waliwatathmini waasisi wa biashara pamoja na mradi kwa kuzingatia vigezo vitano:
- Uvumbuzi
- Mfumo wa Biashara
- Athari kwa Jamii na Mazingira
- Uwezo wa kuvutia Soko
- Timu ya Usimamizi
Ili kuweza kuingia katika 12 Bora kila mshiriki aliyeko fainali alipaswa kuwasilisha ombi kwa mtandao lenye maelezo kwa upana kabla ya kufikia June. Washiriki 24 wa kwanza waliochaguliwa kuingia nusu fainali baada ya hapo walipaswa kutengeneza video yao wenyewe ya kueleza wazo na kushiriki katika mahojiano ya dakika 30 na jopo la majaji kupitia mtandao
“Katika kipindi chote cha changamoto ya Covid cha mwaka 2020, GoGettaz agripreneurs iliendelea kuwa makini na yenye msukumo, sio wakiwa wanajali tu biashara yao na wafanyakazi lakini pia nchi zao na wananchi wenzao pia. Katika kukabiliana na janga la kimataifa walianza kutumia mfumo mpya kukabiliana na mahitaji na changamoto mpya,” Alisema Dickson Naftali, Mkuu wa Generation Africa initiative aliyeko Nairobi. “Washiriki 12 walioingia fainali mwaka huu tayari wana nguvu ya msukumo kwaajili kukua na kuleta mabadiliko katika jamii zao. Biashara zao za kilimo kila mmoja iko tofauti, lakini wote wanachochea bara la Afrika kuwa lenye nguvu katika kilimo”.
WASHINDI WA TUZO YA US$50,000 YA GOGETTAZ AGRIPRENEUR MWAKA 2020
Daniella Kwayu, mwasisi mwenza na CEO wa Phema Agri nchini Tanzania. www.phemaagri.com
Phema Agri ni jukwaa la kidigitali la kilimo linalounganisha wawekezaji wanaotaka kukuza fedha zao kwa kupitia wakulima wadogo wadogo wanaotafuta mitaji ya kufanyia kazi. Kwa kupiti mfumo wao wa crowdfunding (www.phemaagri.com) Taasisi ya Phema Agri iliwaunganisha, iliwaondolea hatari, kuwachumguza na kuwaunganisha na masoko wakulima wanaotafuta wawekezaji. Mwisho wa siku wakulima wanagawana faida na wawekezaji wao. Mfumo huu unafuata mtindo wa biashara wa B2B2C ambao umeunganishwa moja kwa moja na malipo ya banki pamoja na waendeshaji wa simu za mkononi kurahisisha miamala.
“Pengo la kuwezesha kifedha sekta ya kilimo barani Afrika ni US $150 billion kama ilivyokuwa mwaka 2019,” alifafanua Daniella katika maombi yake kwa njia ya mtandao. “Hakuna washindani wa moja kwa moja kwa jukwaa la kilimo nchini Tanzania. Sisi ni taasisi ya kwanza sokoni katika sehemu hii ya sekta. Uwekezaji katika kilimo. Utofauti wetu mkubwa ni uwezo wetu wa kutumia teknolojia kuleta masoko yaliyoundwa kwa usalama, uwekezaji ulioratibuwa vyema kwa njia ya kawaida.”
Phema Agri inakusudia kufikia malengo yake ya kuwawezesha kifedha wakulima milioni moja na kudhibiti minyororo mitano ya thamani katika soko la Afrika Mashariki. Kwa sasa Phema Agri wanafanya kazi katika minyororo miwili tu ya thamani (Minyororo ya thamani ya kuku na nguruwe) wakiwa na lengo la kuongeza thamani zingine za (mahindi, Viazi, Ngano) na kuwapa mafunzo wakulima wengi zaidi kuhusu thamani hizi. Msaada huu wa kifedha kutoka kwenye tuzo za GoGettaz Agripreneur 2020 zitatumiwa kujipatia mikataba ya masoko na tathmini za masoko kwa lengo la kuweka mifumo na kuunganisha wakulima wengi zaidi.
Moses Katala, mwasisi mwenza na CEO wa Magofarm Limited, Mtanzania anayeishi nchini Rwanda. www.magofarms.com
Magofarm Limited inakusudia kutatua changamoto ya gharama zinazoongezeka za vyakula vya mifugo na ongezeko la mahitaji ya upatikanaji endelevu wa viungo vyenye protini na visivyo na athari kwenye uchumi Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la kushughulikia chakula na kilimo (FAO), wafugaji wa kuku kibiashara Afrika wanakumbana na ongezeko la asilimia 20% la bei ya vyakula vya mifugo chenye soya beans na fishmeal kama chanzo cha viungo vyenye protein. Kwa sasa viungo vyenye protein sokoni sio tu kwamba ni ghali kuzalisha lakini pia mzunguko wa uzalishaji wake unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mazingira, alibainisha Katala katika maombi yake ya hatua ya kwanza.
“Vile vile tuko katika azimio la kupunguza upotevu wa chakula katika nchi zinazoendelea,” Alisema Katala. “Upotevu wa chakula una wakilisha upotevu wa rasilimali kama vile ardhi, nishati, maji na vitendea kazi, na hatimae kupelekea katika uzalishaji wa gesi ya ukaa usiyo wa lazima. Kwa mujibu wa FAO, ingekuwa upoteaji wa chakula ni nchi, basi ingekuwa ni nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa zaidi wa gesi ya ukaa duniani baada ya China na USA. Dunia inahitaji suluhisho endelevu la kukabiliana na uharibifu wa chakula. Gharama za kila mwaka za chakula kinachoharibika duniani kinakadiriwa kufika $990 billion”.
“Kwa kuzalisha black soldier fly larvae, Magofarm imejipatia uwezo mkubwa sana wa kupunguza uharibifu wa chakula. Kwa kila tani moja ya black soldier fly larvae tunayozasha kutumia tani 3 za taka za chakula kutoka katika mazingira, ambazo sisi tunazitumia kama malighafi. Kwa kila tani ya fishmeal na Soymeal inayookolewa kutokana na kutumiwa kwa protein zitokanazo na wadudu (magomeal), utunzaji wa mazingira wa kati ya $2,500 na $3,200 kwa kila tani inafikiwa kwa njia ya kuepuka matumizi ya mafuta, matumizi ya ardhi na uzalishaji wa gesi ya ukaa”.
WASHINDI WA $2,500 – TUZO YA ATHARI
Elizabeth Gikebe, Mwasisi mwenza na CEO, Mhogo Foods Ltd inchini Kenya: Mhogo Foods ni taasisi ya ufahamu wa jamii ya kuchakata muhogo na kutengeneza unga wa mhongo usio na gluteni, crisps, wanga na vyakula vya mifugo wakati huo huo ikiwa inatoa mafunzo na kuwasaidia wanawake wanaojihusisha na kilimo kwa kiwango kidogo. www.mhogofoods.com
Millicent Agidipo, mwasisi mwenza na CEO of Achiever Foods Limited inchini Ghana: Achiever Foods iko katika mkakati wa kuokoa maisha kwa kupitia kilimo cha kisasa au cha kioganiki cha Turkey Berries ambazo hutumika kukuza afya ya damu na kuimarisha mfumo wa kinga hasa miongoni mwa wanawake wajawazito. www.achieverfoods.net/en/
Paul Matovu wa Vertical and Micro Gardening (VMG) inchini Uganda: VMG inajenga mashamba ya kujiendesha yenyewe kwa lengo la kufanya kilimo cha mijini kuwa chenye faida kwaajili ya familia zenye kipato cha chini na cha kati . www.verticalandmicrogardening.org
Dysmus Kisilu mwasisi mwenza na CEO Solar Freeze inchini Kenya: Solar Freeze inasaidia kupambana na kuharibika kwa mazao baada ya kuvunwa na wakulima wadogo wadogo wa bidhaa zinazooza kwa haraka kwa kutumia vifaa vya solar vya kuhifazia vyenye baridi na “sharing economy” vifaa mbalimbali vya baridi vya kihifadhia. www.solarfreeze.co.ke
Washiriki wengine 12 wa kwanza wa tuzo ya GoGettaz Agripreneur mwaka 2020:
Fadja Dijou Barry, GoMarkit SL, Sierra Leone. www.gomarkitsl.com
Dexter Tangocci, Integrated Aerial Systems, South Africa. www.iasystems.co.za
Kharbouch Barhoum, Lombrisol, Morocco. www.lombrisol.ma
Brigitha Faustin, Obri Tanzania. www.obritanzania.com
Ifeoluwa Olatayo, Soupah Farm-en-Market Ltd., Nigeria. www.soupah.ng
Agnes Kanjala, The Farm, Malawi. www.thefarmmw.com
JOPO LA MAJAJI 12 WA JUU WA TUZO YA GOGETTAZ AGRIPRENEUR
Eleni Gabre-Madhin
Mwasisi & Afisa Mkuu wa Furaha, bluMoon
Generation Africa Ambassador
Ada Osakwe
Mwasisi & CEO, Agrolay Ventures Nigeria
Generation Africa Ambassador
Ishmael Sunga
CEO, Southern African Confederation of Agricultural Unions
Generation Africa Ambassador
Ellen Cathrine Rasmussen
EVP wa Scalable Enterprises, Norfund
Edson Mpyisi
Mchumi Mkuu wa Fedha & Mratibu wa ENABLE Youth Program, Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank)
Ladé Araba
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika, Convergence Finance
Mwasisi mwenza/Rais wa taasisi ya Visiola Foundation
George Apaka
Lead Agriculture Sector, Mastercard Foundation
Zvichapera Katiyo
Group CEO, Delta Philanthropies, Zimbabwe
WAASISI WENZA NA WASHIRIKA WA KIUFUNDI
Mwaka 2019 international technology group Econet pamoja na global crop nutrition leader Yara, kwa pamoja wali chochea kukua kwa Generation Africa initiative kwa dhumuni la kuwahamasisha na kuwasaidia vijana wajasiriamali wa kilimo Africa na kuleta pamoja taasisi zenye upeo, mashirika na taasisi zinazoshughulika na vijana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo cha chakula Afrika.
Mafanikio ya kampeni ya GoGettaz Agripreneur Prize iliyozinduliwa Davos mapema mwaka 2019 yaliwavutia viongozi wengine katika sekta ya kilimo ulimwenguni na Afrika Mnamo mwaka 2020 Generation Africa initiative iliongeza washirika wengine wanne katika timu yake ya wenye maono: The Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Corteva Agriscience, the Southern African Confederation of Agricultural Unions (SACAU) na the Syngenta Foundation for Sustainable Agriculture.