Home Mchanganyiko WILAYA YA BAGAMOYO HATIMAYE YAZINDUA KLINIKI MAALUMU YA WAGONJWA WA SIKOSELI

WILAYA YA BAGAMOYO HATIMAYE YAZINDUA KLINIKI MAALUMU YA WAGONJWA WA SIKOSELI

0

Baadhi ya Wataalamu wa huduma za ugonjwa wa sikoseli kutoka chuo cha afya (MUHAS) wakiwa katika hospitali ya Wilaya ya Bgamoyo kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu katika kiliniki maalumu ya ugonjwa huo ambayo itakuwa inapatikana kila siku ya jumatatu.

 Mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) Dk. Agnes Jonathan,akitoa elimu kwa baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa wa sikoseli sambamba na kuwaelekea namna ya wazazi kuwahudumia watoto wao pindi wanapokuwa na ugonjwa huo.

Mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) Dk. Agnes Jonathan,akifafanua jambo kwa wazazi, walezi pamoja na wananchi wengine ambao walifika katika kiliniki maalumu ambayo imezinduliwa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa sikoseli katika hospitali ya Bagamoyo.(PICHA ZOETE NA VICTOR MASANGU)

……………………………………………………………………

NA VICTOR MASANGU, BAGAM,OYO

Jopo la wataalam wa Afya kutoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS) kupitia program ya ya selimundu wakiongozwa na Dk. Agnes Jonathan, hatimaye  wameanza rasmi  zoezi la utoaji wa  huduma katika kliniki maalum kwa wagonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.

Lengo la kuanzishwa kwa utaoji wa huduma hiyo imekuja ikiwan imepita  miezi miwili tu tangu Serikali kuzindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa sikoseli mnamo Juni 19,2020  kwa lengo la kuweza kusaidia kutoa huduma kwa wagonjwa mbali mbali wanaosumbuliwa na sikoseli katika Wilaya hiyo.

Katika kukabiliana na ugonjwa huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliagiza  kuanzishwa kwa kliniki maalumu za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuhakikisha watu wengi hasa watoto wanafikiwa kwa urahisi kupatiwa huduma hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Farah alisema kwamba anashukuru sana kwa kuzinduliwa kwa mpango huo ambao utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa ambao wamekuwa wanasumbulia kwa kipindi kirefu  na kusumbuliwa kwa  sikoseli.

“Kwa kweli napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa kuanzishwa kwa utoaji wa huduma hii katika hospitali yetu ya Bagamoyo kwani kutaweza kutoa fursa ya kipekee kwa wananchi wa Bgamoyo kupitia wataalamu ambao wamefika kupata huduma ya matibabu  ya sikoseli ambapo wataondoka  na changamoto ya kwenda kutibiwa sehemu nyingine,”alisema Dk. Farah.

Pia alifafanua kuwa kuzinduliwa kwa kliniki hiyo katika Hospitali ya Bagamoyo kupitia mpango ambao umeanzishwa na serikali kutawapa urahi kwa wagonjwa mbali mbali ambao wanasumbulia na sikoseli kupata matibabau yao kwa uharaka zaidi kuliko na ilivyokuwa katika  kipindi cha mwanzoni.

Naye mratibu wa program ya sikoseli kutoka Chuo kikuu cha afya Muhinbili (MUHAS) Dk.Agnes Jonathan alibainisha kwamba jamii hususan wazazi kuwapelekea watoto wao mapema kupatiwa matibabu ya sikoseli endapo watabaini kuwa anadalili za ugonjwa huo lengo ikiwa ni kumpatia matibabu ya haraka.

“Kumekuwepo kwa baaadhi ya jamii kuwa na mwennendo wa tabia ya kuwa na dhana ptofu kuhusiana na ugonjwa huu wa sikoseli lakini ni vizuri tukajiwekea utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa hospitalini ili waweze kupatiwa matibabu ikiwemo sambamba na kwenda kupima afya zao mara kwa mara,”alisema Dk. Agnes.

Bi. Arafa Said ni Mwanzilishi na Rais wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojulikana kwa jina la Sickle cell Disease Patiebts Community of Tanzania amewaomba wazazi na kuwatia moyo wenye watoto ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huo waondoe hofu na mashaka kwani wakizingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya wanawezeza kusihi maisha marefu bila tatizo.

Mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa Sikoseli ulizinduliwa rasmi Juni 19 mwaka huu na Waziri wa afya maendeleo jinsia wazee na watoto Mh. Ummny Mwalimu katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ukiwa na kauli mbiu inayosema “Huduma bora kwa kila mhitaji, chukua hatua panua wigo.