Mwezeshaji wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya mawasiaino na habari katika uwandishi wa habari za uchunguzi Dkt Pita Mataba akitoa mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari wa redio za kijamii Tanzania yanayofanyika Tunguu kwenye Oisi za TAMWA.(Picha na Masanja Mabula)
……………………………………
Na Masanja Mabula – znz.
WAANDISHI wa habari wa redio za kijamii wametakiwa kuitumia vyema mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupata taarifa zenye uhakika na ukweli.
Mratibu wa mafunzo kutoka shirika la UNESCO Getrude Tatu John alitoa ushauri huo huko Tunguu Ugunja wakati akifungua mafunzo ya siku sita kwa waandishi wa habari wa redio jamii .
Alisema bado waandishi wanakabiliwa na changamoto ya matumizi ya mitandao ya kijamii kuandika habari za uchunguzi na kuwasisitiza kuitumia ili kuongea ubora wa taarifa zao.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Pita Mataba kutoka chuo kikuu SAUTI aliwasisitiza kufanya kazi kwa weledi kwa kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi kwa lengo la kuwalisha waskilizaji wao taarifa Bora.
Matamba alisema uwepo wa teknolojia ya mawasiliano kumerahisha upatikanaji wa taarifa za uhakika na kuongeza kwamba mwandishi anayetumia mitandao ya kijamii habari zake huwa hazina upendeleo.
Nao washiriki wa mafunzo hay walisema yamekuja wakati muafaka na kuahidi kuitumia elimu watakayoipata kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi zao za kuzalisha vipindi na taarifa .
Jumla ya wandishi wa habari 27 kutoa redio za kijamii Bara na Visiwani wanshiriki mafunzo hayo