……………………………………………………………………………
• Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limenunua mitambo mitatu ya uchorongaji yenye teknolojia ya kisasa zaidi kuwahi kutumika hapa nchini. Mitambo hii ina Jumla ya thamani ya TZS Bilion 5.4 (5,347,072,660). Mitambo iliyoagizwa ni mitatu;
1. Lavent 2002 RX-6 Surface Drill Rig kutoka nchini Uturuki yenye thamani TZS 869, 814, 000
2. Christensen’s C140 Surface Drilling kutoka kampuni ya Epiroc Rock Drill AB kutoka Sweden yenye thamani ya TZS 977,067,140
3. Explorac 235 Reverse Circulation Drill kutoka kampuni ya Epiroc Drill AB ya Sweden yenya thamani ya TZS 3, 500,191,520.
Mtambo huu wa Explorac 235 una uwezo wa kujiendesha wenyewe kwa kutumia mfumo wa kompyuta hata opareta akiwa hayupo kwenye mtambo.
Tukio hili la uzinduzi lilfanyika tarehe 15 Septemba 2020 jijini Dar es Salaam.Mitambo hii inaenda kuongeza ushiriki wa Watanzania kupitia Shirika hili la Umma katika uvunaji wa rasilimali madini kwa kuongeza shughuli za utafiti na uchorogaji wa miradi yake na pia kufanya uchorongaji wa kibiashara katika migodi ikiwemo migodi mikubwa. Shirika litaweza kupata mapato zaidi na pia kuingizia Serikali mapato kupitia ulipaji wa kodi mbali mbali na kulipa gawio kubwa zaidi Serikalini.