MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya maji
kujionea namna unavyotekelezwa eneo la Horohoro Mkinga mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt
Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu
zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akieleza jambo wakati wa ziara hiyo kuhusu mradi huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkurugenzi
wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimpokea Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella wakati alipofanya ziara kwenye mradi wa maji wa
Horohoro
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenzi
wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo anayefuatia kwa nyuma ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameitaka Mamlaka ya Maji Safi,Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya
kuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji la Hohorohoro
wilayani Mkinga.
Shigela
aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya maji
kujionea namna unavyotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt
Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu
zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani
Ambapo
mradi huo unatekelezwa na Mamlaka Tanga Uwasa una thamani ya milioni 360 upo kwenye asilimia
85 na mmehaidi asilimia 15 zilizobakia mtakamilisha ifikapo mwisho wa mwezi Septmeba
mwaka
“Ndugu
zangu Tanga Uwasa mnafanya kazi nzuri sana lakini hakikisheni mnatenga fedha
kwa ajili ya kuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji la
Hohorohoro wilayani Mkinga”Alisema
“Lakini
pia Bwawa hili kwa kweli halitoshelezi kama mnavyoona maji yamepungua sana nimeelezwa
kupitia fedha mlizonazo za PFR mhakikishe mnatenga fedha kwa ajili ya
kuimarisha maeneo yanayotorosha maji”Alisema
Hata
hivyo aliwataka pia kuanza upanuzi wa bwawa hilo kupitia force akaunti ili mvua
zitakaponyesha wawe na uhakika wa kuhifadhi maji huku akieleza umuhimu wa
kuhakikisha wanaongeza vilula vya kuchotea maji wananchi kutokana na kwamba
hivi sasa vipo vichache ili kuwaepusha kujazana eneo moja.
“Nizipongeze
mamlaka za Maji Mkoa wa Tanga kwa kuona umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali
yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo
kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani”Alisema RC Shigela.
Hata
hivyo alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya mradi huo ilipofikiwa huku akihaidi
kwenda kukagua kuona kama maji yanatoka Octoba 15 kuja kuona kama maji yanatoka
eneo hilo la Horohoro.
“Kwa
sababu eneo la Horohoro kwetu sisi ni eneo la kimkakati kwa sababu tunataka iwe
ndio iwe habu ya biashara kati ya Kenya na Tanzania watu wanaotaka kufanya biashara
wafike eneo hilo watapata bidhaa kutoka Kenya na Tanzania”Alisema
Awali
akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
alisema Tanga Uwasa wanajenga mradi huo kwa kushirikiana na Ruwasa na umefikia
asilimia 85.
Mhandisi
Hilly alisema wanategemea mpaka ifikapo ndani ya mwezi wa Septemba na Octoba kazi
za msingi zitakuwa zimekamilika na wananchi kuendelea kuhudumiwa kama ilivyopangwa
tangu mwazo pamoja na na kituo cha Forodha cha Horohoro mpakani.
Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
alisema mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa kwa mwisho wa mwezi wa
Septemba mwaka huu watu waanze kunywa maji lakini kwa maboresho ambayo
aliwaagiza kuyafanya watahakikisha yanafanyika kwa fedha kidogo walizopokea.
Alisema
ili wananchi wanapata maji safi na salama ikiwemo kuhakikisha bwawa hilo linauwezo
mkubwa wa kutunza maji kwa kufanyia maboresho kwenye maeneo yaliyoonekana na
changamoto.