RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa pole kwa Watoto na Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Jijini Zanzibar (CCM) Marehemu Salim Hassan Abdallah Turky (Mr.White) baada ya kumaliza kuusalia mwili wa marehemu katika Masjid Noor Mohammad Kwamchina Jijini Zanzibar(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baeraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Didi ya Kiislam Zanzibar katika kisoma cha dua kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae
Jijini Zanzibar Marehemu Salim Hassan Abdallah Turky (Mr.White) kabla ya kuusalia mwili wa marehemu hafla hiyo imefanyika katika Masjid NoorMuhammad Kwamchina na(kushoto kwa Rais) Mtoto wa Marehemu Tofiq Salim Turky,Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Hassan Ngwali na Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal na
(kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Omar Saleh Kabi , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi.wakiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha
hitma.(Picha na Ikulu) WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ya kumuombea
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar CCM Marehemu Salim Hassan Abdallah Turky (Mr.White) baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma kilichofanyika katika Masjid Noor Mohammad Kwamchina Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi, baada ya kuwekwa mwili wa Marehemu Salim Hassan Abdallah Turky (Mr.White) yaliofanyika katika makaburi ya Fuoni Kijitoupele Jijini Zanzibar.(Picha Ikulu)