Home Siasa NDEJEMBI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO, SPIKA NDUGAI ATINGA KUMNADI

NDEJEMBI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO, SPIKA NDUGAI ATINGA KUMNADI

0

………………………………………………………………….

Mgombea Ubunge Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Deo Ndejembi amezindua kampeni zake leo katika Kata ya Dabalo ambapo mgeni rasmi alikua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Spika Ndugai amewaomba wananchi wa Chamwino kumchagua Mgombea wa Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea wa ubunge, Deo Ndejembi na madiwani wote wa CCM ili waweze kuwaharakishia maendeleo.

” Namfahamu Ndejembi, kwa miaka minne Rais Magufuli alimuamini akawa DC wangu wa Wilaya ya Kongwa, amefanya kazi kubwa sana na leo nadiriki kusema maendeleo yanayoonekana yametokana na mchango wake, naombeni mumpe kura akashughulike na changamoto zenu” Amesema Ndugai .

Kwa upande wake Ndejembi amemuahidi Spika Ndugai kuwa atahakikisha Wilaya ya Chamwino inaongoza kwa kura za Rais lakini pia akimhakikishia kushughulika na changamoto za wananchi kwa sababu anazijua.

” Niwaombe ndugu zangu kama ambavyo Chama kimeniamini na nyie mniamini, nina uzoefu wa kujua namna gani nishughulike na Changamoto za Maji, miundombinu na uchumi kwenye Jimbo letu, nawaahidi nitachapa kazi kwa uwezo wangu wote, naombeni mnitume nikawatumikie,” Amesema Ndejembi.