Home Mchanganyiko CORONA YAKWAMISHA KUKAMILIKA KWA WAKATI MRADI WA UZARISHAJI WA UMEME RUSUMO.

CORONA YAKWAMISHA KUKAMILIKA KWA WAKATI MRADI WA UZARISHAJI WA UMEME RUSUMO.

0

Muonekano wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme RUSUMO unaojengwa wilayani Ngara Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda hatua ambayo mradi huo umefikia.

Mafundi wakiwa kazini wakiendelea na ujenzi wa mradi wa kufua umeme RUSUMO eneo ambapo itawekwa mashine za kusukuma umeme yaani (PUMP HOUSE).

Mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme Tanzania TANESCO Alexander Kyaruzi wa kwanza kulia akihoji hatua za ujenzi wa mradi wa kufua umeme RUSUMO kwanini umechelewa kukamilika na kuanza kutoa huduma.

************************************

Na Allawi Kaboyo Ngara.

Mradi wa kufua umeme wa RUSUMO unaojengwa kwa kusimamiwa na nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliotarajiwa kukamilika mwezi februa mwaka huu, umekwama kukamilika kutokana na janga la CORONA baada ya wataalamu wanaojenga mitambo ya kufua umeme huo kuondoka mapema mwaka huu kutokana na gonjwa hilo.

Hayoyamesemwa na meneja wa mradi huo mhandisi Patrick Lwesya wakati wa ziara ya mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme Tanzania TANESCO iliyofanyika leo septemba 14 kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi, ambapo amesema kuwa mradi huo unaendelea vizuri licha ya wataalamu wa masuala ya umeme kuondoka.

Mhandisi Lwesya amesema kuwa baada ya ugonjwa wa CORONA kushamili nchi nyingi zilifunga mipaka yao na wataalamu waliokuwa wakihusika na ujenzi wa mradi huo upande umeme waliondoka ambapo mpaka sasa kazi hiyo ilisimama na kuzorotesha mradi.

“Ujenzi wa mradi huu ulianza mapema kabisa kwenye masuala ya usanifu na kwa mujibu wa mkataba mradi huu ulitakiwa kukabidhiwa mwezi February mwaka huu, hali hiyo imeshindikana baada ya wataalamu wa masuala ya umeme na ufungaji wa mitambo hiyo kuondoka kutokana na ugonjwa wa CORORNA ambao walikuwa wakitoka nchi za Ujerumani na India ambao wamekwama.” Ameeleza Mhandisi Lwesya.

Ameongeza kuwa kwaupande wa ujenzi wa kuta na masuala mengine ya kuongozea maji na maeneo zitakafungwa mashine (PUMP HOUSE) unaosimamiwa na wachina ujenzi wake umefikia asilimia 74 kutokana na wachina hao kutokuondoka baada ya Rais Magufuli kutangaza watu waenedelee na kazi kufatia kuwa kambi zao zilikuwa upande wa Tanzania.

Aidha ameongeza kuwa mradi huu umejenga miundombinu mbalimbali ya maendeleo kwa wilaya za nchi hizo zinazopakana na ujenzi wa mradi ambapo kila wilaya ilipata dola za kimarekani milioni 5 pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliathirika na mradi.

Kwaupande wake mwenyekiti wa bodi ya TANESCO Alexander Kyaruzi amesema kasi ya ujenzi huo yeye pamoja wakurugenzi hawajafurahia kutokana na mradi kuchelewa na kupelekea malengo yaliyowekwa kukwama.

“Nimefika hapa na wakurugenzi kuona maendeleo ya mradi huu, ila hatujafurahishwa na kasi maana ulitakiwa kukamilika mwezi February mwaka huu lakini nilivyoambiwa baada ya wataalamu wa masuala ya mashine na transfoma waliondoka ila kwasasa wamerudi kati ya kesho wataanza kazi licha ya kuwa tumeambiwa kuwa bada ya shughuri zote kuendelea mradi unatajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka kesho 2021.” Amesema Kyaruzi.

Kyaruzi amsema kuwa mradi huo ukikamilika utazarisha mega wat 80 ambapo kila nchi mwanachama itachukua mega wat 27, na kuongeza kuwa mradi huo umeweza kuwanufaisha wananchi wan chi hizo kwa kuwapatia ajira za muda na wengine za kudumu lakini pia wananchi wanaozunguka mradi wameweza kufanyabiashara na kukuza uchumi.

Mradi wa kufua umeme RUSUMO unajengwa kwa mkopo kutoka benki ya dunia wa kiasi cha shilingi milioni 340 dola za kimarekani ambapo Tanzania italipa mkopo huo kwa asilimia 100%, Rwanda asilimia 50% huku Burundi ikiwa hailipi chochote na asilimia iliyobaki kutolewa kama ufadhili.