Wakazi wa vijiji vya Mundindi,Amani na Nkomang’ombe na maeneo mengine yenye hazina kubwa ya Madini ya Chuma na Mkaa wa Mawe ardhini wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kulipa fidia ya zaidi ya bil 12 na kuanza uchimbaji katika migodi hiyo ili iweze kuleta tija kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Wakazi hao ambao wameshapisha maeneo ya migodi wakisubiri fidia serikalini wanasema ni vyema serikali ijayo ikafungua mgodi wa chuma na mawe wilayani humo na kisha kutoa vibali kwa wachimbaji wadogo .
Wakizungumza wakati wa uzinduzi kampeni za chama cha mapinduzi jimbo la Ludewa akiwemo Petro Mwangombe na Joseph Maganga wanasema suala la machimbo ya Liganga na mchuchuma limekuwa likizungumzwa kwa kipindi kirefu hivyo serikali ijayo ione ulazima wa kuanza machimbo hayo.
Wamesema endapo serikali itaanza uchimbaji wakazi watainua uchumi kwa kuuza bidhaa mbalimbali za chakula na ajira huku serikali nayo ikipata fedha nyingi za mapato yatokanayo na machimbo
“Tunaomba serikali ilipe fidia kwa kuwa tulishapisha maeneo yetu baada ya kuahidwa kulipa fidia kwasababu hatua tunachokifanya katika maeneo yake tena” Alisema Joseph Maganga.
Awali akifafanua vipaumbele vyake mgombea ubunge jimbo hilo Joseph Kamonga anasema muda mfupi baada ya kuapishwa atafuatilia suala fidia kwa maeneo yote yanayopitiwa na migodi na ujenzi wa barabara huku pia akigusa sekta ya kilimo na uvuvi katika ziwa nyasa kwalengo la kufungua milango ya uchumi ludewa.
Kamonga amesema wana Ludewa wanapaswa kuwa na subira wakati serikali inaweka utaratibu mzuri wa kimikataba na kwamba katika kuweka miundombinu rafiki ya machimbo tayari ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Zege umeanza kufanyika huku katika usafiri wa majini nao ukianza kuboreshwa .
“Mapema baada ya kuapishwa nitafuatilia kwa ukaribu fidia ya zaidi ya bil 12 kwa wakazi wa Nkomang’ombe na Mundindi na kufanya kila jitihada katika uboreshaji wa sekta ya kilimo, barabara na uvuvi” Alisema Joseph Kamonga.
Nae mkuu wa wilaya katika kukuza uchumi wa Ludewa na utatuzi wa baaadhi ya changamoto zake mkuu wa wilaya hiyo Andrew Tsere anasema shule tano za sekondri ikiwemo Ulayasi,Madunda,Lugarawa na Ikovu zimetengwa kutoa elimu ya kilimo ili kuinua uchumi huku masoko na miundombinu ikiendelea kuboreshwa.