Mgombea ubunge jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga akiomba kura
Baadhi wa wananchi walihudhuria uzinduzi huoWazee wa kabila la wahehe wakimsimika Jackson Kiswaga kuwa mmoja wa machifu wa Kabila hilo na kutoa baraka za kuchaguliwa kuwa mbunge.
**********************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa kwa tiketi ya CCM, Jackson Kiswaga amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua kuwa mbunge ili aweze kutatua changamoto za jimbo hilo na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni wa jimbo hilo uliofanyika katika kijiji cha Kalenga, Kiswaga alibainisha changamoto mbalimbali za jimbo la Kalenga na endapo wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao atahakikisha anakabiliana nazo kuweza kuzitatua katika kipindi cha ubunge.
Kiswaga alisema kuwa anafahamu changamoto zinazoikabili jimbo la Kalenga na vilio vya wanakalenga hivyo atahakikisha changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazo zimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha anatatua kero hiyo.
Alisema kuwa anafahamu kwamba barabara ya kwenda mbuga za wanyama ilivyo na changamoto kubwa kwa sasa hivyo endapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kusaidiana na serikali ili kuweza kusukuma maendeleo ya Kalenga.
“Katika kipindi kilichopita kulikuwa na mvua nyingi hivyo nafahamu kabisa suala la miundo mbinu kuwa na changamoto na mimi nikiwa mbunge litakuwa jambo la kwanza ambalo nitalifanyia kazi kuhakikisha kwamba tunarekebisha miundo mbinu yetu ili iweze kupitika ili kuweza kusafirisha mazao yetu vizuri.” Alisem
Kiswaga alisema kuwa anafahamu jimbo la Kalenga linakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya kwani sehemu nyingi tumeweza kujenga vituo vya afya na zahanati lakini havijakamilika hivyo moja mambo ambayo yatafanyiwa kazi endapo nitachaguliwa kuwa mbunge kuwa na vituo vya afya vinakamilika.
Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta yaElimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya shule, kujenga hostel za wa wanafunzi ambao wamekuwa wakipata shida hasa mabinti hivyo kwa imani ya wananchi atahakikisha sekta ya elimu inakuwa zaidi kuliko ilivyokuwa awali na kuhakikisha mazingira ya walimu na wanafunzi yanaboreshwa.
“Sekta ya elimu inakabiliwa na upungufu wa walimu, upungufu wa madawati na nafahamu watoto wetu wa kike wanapata mimba katika shule zetu za sekondari hivyo miongoni mwa mambo nitakayoyasukuma ni kuhakikisha tunajenga hosteli ili kupunguza changamoto ambazo dada zetu wanapata.
Kiswaga alisema kuwa anafahamu changamoto wanayokabiliana nazo vijana katika sekta ya ajira, walemavu na wakina mama kuhusu mikopo mbalimbali hivyo kwa kupitia halmashauri kupitia asilimia kumi inayotengwa kwa ajili ya hayo makundi zinawafikia kwa wakati kuweza kuinua uchumi wao.
Aidha Kiswaga alisema kuwa anafahamu changamoto wanayokabiliana nayo wakulima katika suala la kilimo hasa kuhusu pembejeo hivyo endapo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha changamoto hizo zinakwisha na wakulima kuweza kunufaika na kilimo kuweza kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla.
Akizungumzia changamoto ya umeme Kiswaga alisema kuwa atahakikisha vijiji vinanufaika na mradi wa REA kwa kupata umeme ili kuweza kuharakisha maendeleo kiuchumi kwani serikali iliyoko madarakani imepambana vyema kuwaletea maendeleo wananchi.
Kiswaga aliwataka wananchi kuwabeza watu wanaopita na kusema kwamba serikali ya CCM haijafanya kitu na kuwataka kuwachagua viongozi wa CCM kwenye ngazi zote kuanzia nafasi ya Urais ambapo John Magufuli amesimama kwenye nafasi hiyo, wabunge na madiwani ili kuweza kupata utatu wa maendeleo.
Naye Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo, uliopambwa na msanii wa bongo fleva, Stamina, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Dk.Abel Nyamahanga aliwaomba wananchi wa vyama vyote nchini kukichagua chama cha Mapinduzi kupitia wagombea wa nafasi zote kuweza kuwaletea maendeleo wanayotaka.
Dr. Nyamahanga aliomba ananchi wa jimbo la Kalenga kuhakikisha wanampa kura nyingi za ndio mgombea urais John Pombe Magufuli na Mgombea Ubunge Jackson Kiswaga na madiwani katika kata zote za Kalenga ili kupata utatu ambao utawaletea maendeleo katika jimbo hilo
Baadhi ya wagombea ubunge kwenye kura za maoni kwenye jimbo hilo waliungana akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake Godfrey Mgimwa ambao waliwaomba wananchi kukiunga mkono chama cha Mapinduzi (CCM) kuwachagua madiwani wabunge na mgombea wa Urais John Magufuli.