Home Mchanganyiko NMB MARATHON YALETA NEEMA YA SH. MILIONI 100 KUSAIDIA WATOTO WENYE UGONJWA...

NMB MARATHON YALETA NEEMA YA SH. MILIONI 100 KUSAIDIA WATOTO WENYE UGONJWA WA SARATANI

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi wa Mbio za NMB Marathon baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, wa nne kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki , wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB Ruth Zaipuna wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam kufungua Mbio za NMB Marathon na kutoa zawadi kwa washindi, wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Sh. Milioni 100 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati alipohitimisha Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Baadhi ya washiriki wa mbio za NMB Marathon.

……………………………………………………..
NA, NOEL RUKANUGA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha mbio za NMB Marathon za kilomita 5 , 10 na 21 na kufanikiwa kukusanya Sh. 100,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi mbio za NMB Marathon Mhe. Majaliwa, amesema kuwa wadau wanatakiwa kuendelea kujitokeza kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutoa elimu.
”Ninawapongeza wote walioshiriki mbio za kiliomita 5, 10 na 21 na kumaliza salama, kwani ushiriki wenu ni fursa kwa kufanikisha kukusanya Sh. 100,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa saratani” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa NMB wameonesha nia ya kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya michezo pamoja kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kujinga na bima.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa Hospitali za Rufaa zinazotoa huduma kwa wagonjwa wenye Saratani kutenga wodi maalumu kwa ajili ya watoto wenye saratani ili kupunguza ahueni ya matibabu.
Katika hatua nyengine ametoa wito kwa watanzania kujiunga na bima, kutokana na mwitiko kuwa mdogo.
”Nimefurai kusikia benki ya NMB imeuunganisha nguvu ya pamoja kwa kutoa elimu ya bima kwa jamii kwa kushirikiana na mashirika mengine ya bima” amesema Mhe. Majaliwa.
Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB Ruth Zaipuna, amesema kuwa wamefanikuwa kudhamini mbio hizo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha watu kuwa na uelewa kuhusu muhimu wa kujiunga na bima, kuendelea kutoa elimu ya afya, kuchangia fedha ya matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa saratani pamoja na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.
Zaipuna ameeleza kuwa kupitia NMB Marathon wamefanikiwa kukusanya Sh. 100,000,000 kwa ajili ya wasaidia watoto wenye ugonjwa wa saratani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Miseru, ameishukuru Benki ya NMB kwa kutoa sh. 100,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa saratani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi na katika mbizo za NMB Marathon na kufanikwa kugawa zawadi kwa washindi katika mbio za kilomita 5, 10 na 21.