Home Mchanganyiko NHIF ZANZIBAR YAHAMASISHA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA NA MAZOEZI

NHIF ZANZIBAR YAHAMASISHA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA NA MAZOEZI

0

MENEJA
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta
akizungumza wakati wa Bonanza la michezo kwa watumishi wa Serikali na
wananchi Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja vya Mau mjini Unguja

MENEJA
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta katikati
akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa bonanza hilo

Washiriki wa Bonanza hilo wakiendelea na mazoezi kwenye viwanja hivyo

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye bonana hilo

 

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar umehamasisha wananchi kujiunga na
mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa
sambamba na ufanyaji wa mazoezi kila wakati kwa ajili ya kupambana na
magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu.

Hayo
yalisemwa na Meneja Mkaazi wa ofisi ya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Zanzibar Ismail Kangeta wakati akitoa elimu ya umuhimu wa bima ya
afya wakati wa bonanza ambalo liliandaliwa na Mfuko huo ofisi ya
Zanzibar.

Bonanza
hilo lilikwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima
ya Afya pia kusisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye michezo ili
kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ndio yamekuwa tishio kwa afya
za watu kwa sasa.

“Kama
unavyojua ukifanya mazoezi mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa wa
kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ndio maana tumeona
tuandae bonanza hili na litakuwa linafanyika kila wakati”Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunifaika na huduma mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitoa