Home Siasa MGOMBEA WA CCM EXAUD KIGAHE ATAJA VIPAUMBE NANE VYA MAENDELEO JIMBO LA...

MGOMBEA WA CCM EXAUD KIGAHE ATAJA VIPAUMBE NANE VYA MAENDELEO JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

0

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe akiomba kura kutoka wanachi wa jimbo hilo

Mamia ya wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kamapeni za mgombea ubunge wa Jimbo hilo.
 

Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za nane kwa
wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamapeni za
kuomba kura kwa wananchi wa jimbo la Mufindi,Exaud Kigahe alisema kuwa jimbo la
Mufindi Kaskazini linakabiriwa na changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazo
zimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge
atahakikisha anatatua kero hiyo.

Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta ya
Elimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya shule,kuanzisha  mashindano ya kumpata mwananfunzi bora na
mwalimu bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwa
wastani mzuri.

“Wananchi wa jimbo la Mufindi wengi ni
wakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya kilimo kwa kuwa hata mimi nimekulia
kwenye family ya wakulima hivyo nitahakikisha kuwa tunaboresha masoko ya
wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri” alisema Kigahe

Aidha Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na viwanda,afya,biashara,umeme na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwa
mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

 

“Kazi kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu na
niwahakikishie sisi wabunge watatu wa Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi)
tutafanya kazi kwa pamoja kwa kuwa  lengo
kubwa ni kuleta maendeleo”alisema  Kigahe

 

 

Lakini pia Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
Ameshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Mufindi Kusini na Kuwaomba Wananchi
kuhakikisha Wanampa kura Za Kishindo Mh Rais, mbunge,Madiwani wote waCCM.

 

Naye Katibu Wa CCM Wilaya ya Mufindi Mgego amewahakikishia Kuwa
chama cha mapinduzi kitapata ushindi wa Kishindo hivyo wanaCCM wanatakiwa kuwa
mstari wa Mbele kutafuta kura za Mh Rais,Wabunge na Madiwani wa CCM.

 

 

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa Dr Abel Nyamahanga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa
kampeni hizo aliwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuhakikisha
wanampa kura nyingi Mgombea Ubunge Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kwa kuwa
ameamini na Rais.