Home Michezo ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA 3-0 FULHAM UGENINI 

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA 3-0 FULHAM UGENINI 

0
Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London PICHA ZAIDI SOMA HAPA

……………………………….

ARSENAL imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham waliorejea msimu huu, mabao ya Alexandre Lacazette dakika ya 18, mchezaji mpya Gabriel Magalhaes dakika ya 49 na Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 57 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
Huo ni mwendelezo mzuri wa matokeo ya timu chini ya kocha Mikel Arteta msimu mpya, wakitoka kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatyia sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Liverpool Agosti 29 Uwanja wa Wembley Jijini London.