Pongezi kwa mfungaji wa mabao yote hayo, mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube aliyefunga dakika za 69 na 89.
Dube aliyesajiliwa kutoka Highlanders FC ya Bulawayo, bao la kwanza alifrunga akimalizia pasi ya winga Iddi Suleiman ‘Nado’ na la pili alimalizia pasi ya Mzimbabwe mwenzake, kiungo mshambuliaji Never Tigere.
Kwa ushindi huo, Azam FC inayomilikiwa na Bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi sita na kupanda kileleni, ikiwazizi pointi tatu mabingwa watetezi, Simba SC amnao nap kesho watacheza mechi ya pili.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Gwambina FC ililazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
Ligi Kuu itaendelea Leo kwa mechi tatu, JKT Tanzania wakimenyana na Dodoma Jiji FC kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, Mtibwa Sugar na Simba SC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na KMC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
Kesho Ihefu itawakaribisha Ruvu Shooting kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Biashara United watamenyana na Mwadui FC kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Karume Musoma mkoani Mara na baadaye Saa 1:00 usiku, vigogo Yanga SC watamenyana na Mbeya City Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja tu wa kukamilisha Raundi ya pili, Namungo FC wakiwaalika Polisi Tanzania kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.