Home Siasa KAMPENI ZA CCM ZAWAKIMBIZA WAPINZANI NJE YA NCHI

KAMPENI ZA CCM ZAWAKIMBIZA WAPINZANI NJE YA NCHI

0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, leo Ijumaa Septemba 11, 2020

(NA JOHN BUKUKU-CHATO-GEITA)

……………………………………….

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi (CCM) Ndugu Hamphrey Polepole amesema kuwa kwa miaka mitano wamejenga Taasisi imara ya Chama cha Mapinduzi yenye uwezo kwa maana ya makada madhubuti wanachama wameimarika na idadi ya wanachama imeongezeka mara dufu.

Polepole ametoa Kauli hiyo  leo mjini Chato Mkoani Geita wakati akizungumza na vyombo vya habari kutoa taarifa kuhusiana na maendeleo ya kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Aidha Polepole amesema kuwa Nchi wameishika na kila wanapofika inasimama kwa sababu Watanzania wamekubali kazi nzuri sana ambayo imefanyika katika nchi ya Tanzania  chini ya Rais. Dk. John Pombe Magufuli, kule Zanzibar pia wanakwenda vizuri mnoo.

“Mzee Kikwete tumemuweka pale Lindi, kama kuna watu wanavuruga pale yeye anawafahamu vizuri, ukiletewa mjanja wako ndiyo kama mambo yanayoendelea, leo hii tumegundua mgombea mmoja ameshaondoka Nje ya nchi kwa sababu mambo yameshafika shingoni” ameweka bayana Polepole.

 “Wanasema watatoa Bima ya Afya kwa wananchi wote, niwaulize; Unaweza kutoa Bima ya Afya wakati huna Hospitali? Unaweza kupanda mbegu katika shamba ambalo hujaliandaa? Sisi tumeongeza fedha ya dawa, vifaa tiba, miundmbinu ya hospitali, tumeajiri madaktari,” ameeleza Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akionesha Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 wakati akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, leo Ijumaa
Septemba 11, 2020

Picha zikionesha waandishi wa habari mbalimbali wakifuatilia na kunukuu kile alichokuwa akizungumza Ndugu Humprey Polepole.