Soko la simu Tanzania lazidi kuchangamka baada ya brand nyingi za simu kuleta matoleo mbali mbali yenye sifa tofauti tofauti. Kupitia kurasa za mitandao ya Kijamii ya Infinix Mobile Tanzania, tumegundua kuna ujio wa Simu mpya aina ya Infinix ZERO 8 yenye sifa kubwa kuliko simu zao nyingi.
Ikumbukwe Infinix wameendelea kulishika soko kupitia simu yao aina ya Infinix NOTE 7 na sasa kuja na Infinix ZERO 8, Inasemekana simu hii itakuwa na uwezo mkubwa wa Camera, RAM na ROM kuliko simu zao zote walizowahi kutoa, yani hii ndio flagship yao kwa mwaka huu. Simu itakuwa na camera 4 zenye 64MP hivyo kupata picha nzuri kama professional Kamera
Simu hii imeshafika baadhi ya nchi Africa ikiwemo Nigeria na Misri na inatarajiwa kufika katika soko la Tanzania mapema mwezi huu wa Tisa.
Je kutokana na sifa za simu hii ya Infinix ZERO 8, itauzwa bei gani?