Yanga SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata dakika ya saba, mfungaji Lambert Sibiyanka akimalizia pasi ya Jeremiah Juma.
Mshambuliaji mpya, Mghana Michael Sarpong akaisawazishia Yanga SC dakika ya 19 baada ya kutokea tafrani kwenye lango la Tanzania Prisons.
Tanzania Prisons ilimpoteza beki wake tegemeo, Nurdin Chona aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu mshambuliaji mwingine mpya, Yacouba Sogne kutoka Burkina Faso.
Mechi zilizotangulia, mabingwa wateteezi Simba SC waliuanza vyema msimu mpya baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu SC iliyopanda daraja Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Dodoma Jiji FC wakashinda 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mtibwa Sugar ikalazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting ya Mlandizi, Pwani Uwanja wa CCM Shabiby, Gairo mkoani Morogoro, Namungo FC ikashinda 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na Biashara United wameshinda 1-0 dhidi ya Gwambina FC Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
Mechi za kwanza za Ligi Kuu zitakamilishwa Leo kwa KMC kuwaalika Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Kagera Sugar kuwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na Azam FC kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikhalo, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya/Tonombe Mukoko dk75, Farid Mussa/Tuisila Kisinda dk46, Feisal Salum, Michael Sarpong, Ditram Nchimbi na Deus Kaseke/ Yocouba Sogne dk46.
Tanzania Prisons; Jeremiah Kisubi, Michael Mpesa, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya/Kassim Mdoe dk74, Lambert Sibiyanka, Mohamed Mkopi, Jeremiah Juma/Samson Mbagula dk46 na Adilly Buha/Ezekeia Mwashilindi dk50.